Babuu wa Kitaa kurudi tena kwenye muziki.

Babuu wa Kitaa kurudi tena kwenye muziki.

Kimbia akiwa akiwemo Langa na Mchiz Mox ni wimbo wake Babuu wa Kitaa ambao ni moja ya nyimbo bora za hiphop tulizonazo.

Lakini Babuu kwa muda mrefu sasa amekuwa ni mtangazaji katika kituo cha Clouds Tv, hivyo muziki aliupo kisogo.

Mapema leo kupitia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv mdogo wake ambaye ni Country Boy amesema “Baada ya Ramadhani Babuu anarudi tena kwenye muziki.

Na anarudi kisasa zaidi mimi na Young Lunya tumeshilikiana katika kuandika wimbo wake ili kumleta na unyama wa sasa.

Sisi Tizneez imani yetu ni kubwa katika ujio wake kulingana na upekee wa midondoko yake Babuu wa Kitaa lakini mtaji wa sauti yake.

#TuzungumzeMuziki