BABU TALE AMSIFU NASH MC

babu

BABU TALE AMSIFU NASH MC

Babu Tale ni moja kati ya wadau wa muda mrefu ambaye sasa amemshikiria Diamond Platunumz lakini pia kundi zima la Tiptop Connection ambalo lina wakali kama Madee,Tunda Man, Dogo Janja na wengine wengi.

Kupitia mtandao wa picha instagram Babu tale alimpost Nash mc na kumpa sifa zake ambapo ameandika”Acha leo niwe msemakweli kuhusu @maalimnash ni mwana hip hop wapekee ninaemkubali ambae ngoma zake hakuna hata neno moja la kizungu hii inaitwa tamaduni music asante kaka mungu akuongoze @maalimnash

Nash Mc ni moja kati ya wasanii wakongwe wa hiphop wenye misimamo hasa katika muziki huo wa hiphop. Nash mc aliwafanya vyema na nyimbo zake kama Tabia, Hasi 15,Naandika,Maswali ya kiwaki,Asiyehusika na hiphop pamoja na nyingine nyingi.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez