Baada ya kukaa sober house siku 28 Chid Benz adaiwa kutoroka

chidbenz

Baada ya kukaa sober house siku 28 Chid Benz adaiwa kutoroka

We all know that rapa mkali wa Ilala Chid Benz, alikuwa kwenye matibabu ya kupambana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya huko Bagamoyo.

taarifa mpya ni kwamba rapa huyo ametoroka katika jumba hilo baada ya kukaa kwa siku 28 pekee.

Akizungumza na Global Publishers meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura, amethibitisha kuondoka kwa Chidi akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu.

“Ni siku 28 tu alikaa, lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Tumaini.

Aliomgeza, “Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka aling’ang’ania kuondoka naye. Sisi pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa,”

Pia Global walimtafuta Chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.

Tabu Tale alipoulizwa kuhusu mwala hilo alisema: “Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu Chid, muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

Source Times Fm www.timesfm.co.tz