BAADA YA FREEDOM MR II SUGU AINGIA TENA STUDIO

IMG_2828

BAADA YA FREEDOM MR II SUGU AINGIA TENA STUDIO

Freedom ni wimbo wake ulitoka mwaka jana ambao alimshirikisha Mr Blue, na wimbo huo ulitengenezwa katika studio za Mj Record chini yam kali Marko Chali.

Licha ya wimbo kuwa mzuri na Mr II Sugu kuonyesha uwezo wake katika game ya hiphop hapa nchini Tanzania lakini wimbo huo ulikosa nafasi katika media, ila ulifanya vyema katika blog mbalimbali hususani Tizneez.com kwa kupata upakuaji wa watu wengi.

Mapema kupitia mtandao wa picha Mkongwe na godfather wa muziki wa kizazi kipya alipost picha ikimuonyesha akiwa katika chumba cha kurekodi ambapo aliandika “Strictly to my fans# Leo nilipita MJ Records nawatolea kitu kidogo # Mmeniulizia kwa muda mrefu sana sasa”

Sugu kwa sasa ni Mh Mbunge wa Mbeya Mjini na jina lake kamili Ni Joseph Mbilinyi, ambaye pia ni msanii aliyetetea na kupigania mengi katika muziki huu ambao leo umekuwa ajira ya watu wengi.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez