Azma Mponda Aeleza alivyoweza kufanya kazi na Mr II Sugu.

Azma Mponda Aeleza alivyoweza kufanya kazi na Mr II Sugu.

Garagasha ni wimbo wa Azma Mponda ambao amemshirikisha  Izzo Biznes, Abela na Mr II.

Mr II Sugu sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA ambaye anatambulika kwa jina la Mh Joseph Mbilinyi.

Licha ya kuwa Mh Mbunge lakini ameendelea kujishughulisha na mambo yanayohusu muziki kila leo.

Mapema leo Azma hakuacha kuweka wazi jinsi ambayo aliweza kufanya kazi na Mh Joseph Mbilinyi ambapo Azma amesema “Nilifanya wimbo huu wa garagasha nikamtumia audio yake, kiukweli akapenda na akasema yuko tayari kufanya. Na akaenda mwenyewe studio na wala sikuwepo akarekodi.

Ila katika kufanya video ndiyo kulikuwa na vikwazo kadhaa lakini ni kwa sababu ya mikutano ya uongozi wake tu, kwaiyo video tulilzimika kuacha kufanya mara tatu.

Ila katika mara nyingine tuliweza na Sugu alifika eneo ya kufanya video mapema kuliko watu wote, alifika saa 7 mchana wakati video ni saa 10 jioni. Kiukweli nashukuru kufanya kazi na Mr Sugu.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa