‘Asiye na kumi ana moja’ Mapacha Maujanja Saplaya.

‘Asiye na kumi ana moja’ Mapacha Maujanja Saplaya.

Uamuzi wa kutoa album na kuuza wenyewe ni tendo la ushujaa mno, wakati huo watangazaji wengi wasiojua hata maana wala umuhimu wa album wameendela kuwamezesha uongo wasanii wengi ambao bado wamebaki kuwa chipukizi kwa kukosa album.

Mapacha Maujanja Saplaya ni muunganiko wa Kulwa na Dotto ambao ni moja kati ya wasanii wachache waliopigania haki za kimuziki katika muziki huu wa kizazi kipya na hata kutoa umungu mtu kwa baadhi ya wadau na watangazaji ambao hujiona wao ni zaidi ya kipaji cha msanii.

Ghetto love ni album yao ambayo wameitoa sasa, tena wameitoa wakati ambao wala hawafanyi vizuri katika anga ya radio na runinga isipokuwa mtaani.Hii imeleta utofauti katika muziki maana wengi husubiri wakati akifanya vyema ndio atoe album.

Kujiamini kwao ndio mtaji wao, wakati wengine wakiendelea kulalama kuhusu wadau kadhaa na wapambe wa muziki wao wameamua kutoa album yao na kuamua kuuza yenyewe mkononi.

Ama kweli asiye na kumi ana moja. Ni wazi Mapacha wamegundua thamani yao na jinsi ya kuweza kujipatia kipato kwa njia ya mauzo album yao moja kwa moja kwa mashabiki wao.

Mapacha wameonyesha miaka hii sio miaka ya kusubiri mpaka mdau, bali ni vyema kutambua thamani yako  kwa asilimia moja ili uweze kuendeleza maisha yako kupitia muziki wako.

Pia mashabiki muda ni huu wa kuonyesha  umuhimu katika kuwawezesha Mapacha isiwe katika maneno tu bali iwe vitendo zaidi.

Na kama unahitaji album ya Mapacha Maujanja Saplaya wapigie kupitia namba hizi 0713 23 32 03 au 0712 71 57 05

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez