ALLY KIBA ASIKITISHWA NA MEDIA ZA TANZANIA

e9486ce80ab9c6d4e4be3d329d1f463c

Ally Kiba ni moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kwasasa ndani na nje ya Tanzania,Pia ameshiriki katika msimu wa coke studio mwaka huu ambapo amepata fursa ya kushiriki katika wimbo mmoja na star Neyo kutoka nchini Marekani

Kupitia mtandano wa picha Instagram Ally Kiba alielezea masikitiko yake juu ya media kupotezea project ya Peace one day ilimkutanisha na wakali  wengine wa Afrika kama,Ice Prince,Mafikizolo na wengine wengi.Tamasha hilo lilifanyika jana katika viwanja vya Amohoro jijini KIgali Rwanda

Ally Kiba ameandika”Hii Ni Kwa Vyombo Vya Habari Ambavyo Havijatoa Ushirikiano Katika Kampani Ya Peace One Day .
Next Time Fanya Kwaajiri Ya Tanzania Sio Kwasababu Ya Alikiba Au Mtu Yoyote Atakae Wakilisha TANZANIA ,Kwasababu Mimi Nibinaadam Sijakamilika Naweza Kua Nimekukosea Bila Kujua Au Kwa Kujua pia .
Haijalishi Kwasababu Nchi Yetu Ina Amani Ndio Muache Kutoa Ushirikiano Kumbukeni Tupo Kwenye Kipindi Kigumu Cha Uchaguzi Naomba Mungu Atunusuru Kwa hilo Lakini Pia Inaleta Picha Mbaya Kwa Nchi ZaJirani Zenye Machafuko Kuona Hatutoi Ushirikiano. Kwahiyo Haipendezi Kwa Kweli
Kuna Wapenzi Wa Kazi Yangu Wamelalamika Sana Kila Kona Ya Dunia Kuhusu Kampani Ya Peace One Day
Kwanini Hamkuona Hilo !! Imeniuma”#PeaceOneDay #Amahoro #KingKiba

Unaweza kuwa rafiki yetu

facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez