ALI KIBA “SIWEZI KUMUITA WALA KUMFANISHA MTU NA MNYAMA”

alikiba
Kwa kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu Ruby na Ali Kiba ambapo msanii wa bongo fleva Ruby kusema kuwa Ali Kiba amemuita mbwa.
Kupitia katika post hiyo kwenye mtandao wa kijamii Instagram Ali Kiba amemjibu Ruby katika post yake aliyoweka iliyotoa shutuma hizo.
Ali Kiba ameandika “Nimependa tu jina mdogo wangu sikuwa na sababu yoyote inayokuhusu wala kufikiria kama nitakuudhi, kutumia jina la Ruby.Mimi kama kaka yako kiumri na kimuziki pia kutoka moyoni naomba msamaha kwa kutumia jina hilo.Pia unaelewa ni jinsi gani nafurahishwa na nyimbo zako ukiachilia hilo, mdogo wangu mimi nawashukuru wazazi wangu kwa malezi waliyonilea vizuri kwahiyo siwezi kumuita mtu wala kumfaninisha yoyote na jina lolote la mnyama.Ukisikiliza vizuri interview utaelewa.Naomba unisamehe mdogo wangu sikumaanisha hivyo .Ubarikiwe #kingkiba”

www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez