ALI KIBA AELEZA KILICHOLETA TOFAUTI NA SAUTI SOUL

alikibaa

ALI KIBA AELEZA KILICHOLETA TOFAUTI NA SAUTI SOUL

Unconditionally bae ni wimbo wao wa pamoja unaofanya vyema katika radio na runinga ndani ya Africa sasa. Wimbo huo ambao ulitoka mapema mwezi mmoja uliopita na wengi kuonekana kuupenda katika siku chache tangu kutoka kwake.

Licha ya wimbo huo kuonekana kushika kasi, lakini ilileta maneno mengi baada ya msanii Ali Kiba kuonekana kutoshare katika mitandao ya kijamii kuhusu wimbo huo.

Mapema leo Ali kiba hakusita kuweka wazi kile ambacho kilikuwa kinaendelea kati yake na Sauti Soul. Ambapo Kiba amesema “Ni vitu vidogo tu viliingiliana na vilikuwa nje ya makubaliano yani mkataba, mkataba ulikuwa na 50 50 kila upande. Hivyo kulitokea kukiukwa kwa makubaliano kati yangu na wao, ila mwisho wa siku makubaliano yakafutwa hivyo hakuna tatizo mambo yote yako sawa.

Ali kiba sasa anafanya vyema na wimbo wake wa Lupela ambao umeendelea kushika chati mbalimbali za radio na runinga ndani na nje ya nchi.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez