Afande Sele Amuandikia ujumbe Darasa

darasa

Afande Sele Amuandikia ujumbe Darasa

Kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ Mfalme wa pekee katika muziki wa hiphop hakusita kumuandikia ujumbe msanii Darasa ambaye kwa sasa ndiye msanii mwenye wimbo unaofanya vyema katika vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, kwenye kumbi za starehe na kwingineko.

Afande Sele ameandika ‘ Mtu yeyote anaetumia AKILI katika jambo lake mara nyingi hufikia malengo…wapo madogo zangu wengi wakali sana…mimi wote nawakubali lakini umuhimu wa kipekee nampa @darassacmg ‘El Classico Darasa’ leo hii ni kwa sababu kaja kukanusha uzushi na upuuzi wa kuiaminisha jamii kwamba hiphop imekufa kiasi cha wengine kuthubutu kuinajis hiphop kwa kuilinganisha na singeli…Roho saba katika moja ya mistari yake ndani ya wimbo Nakupenda hiphop anasema’Hiphop ndio mziki na hili lake biti…Amba nipe kiki niwabastie mamluki….Nakupenda Hiphop…Nakuheshimu @darassacmg ….Here we go bro’