“Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes” Solo Thang

“Afande Sele alistahili ufalme wa Rhymes” Solo Thang

Mpambano wa kutafuta mfalme wa Rhymes ulifanyika mwaka 2004, ambapo mpaka leo haujawahi kuendelea tena tangu mwaka huo. Ila msanii aliyebahatika kuchukua taji hilo ni Afande Sele.

Mashabiki wengi wamekuwa wakiamini kuwepo kwa chuki kwa Solo Thang kwenda Afande Sele tangu kuisha kwa mpambano wa Mfalme wa rhymes mwaka 2004.

Kilio changu ni wimbo wake Solo thang, na wimbo  huu uliozungumzia tukio zima la shindano hilo. Na kila shabiki alikuwa na maana yake kichwani mwake. Lakini pia Solo hakuacha kusema hata iweje hatokuja kushiriki katika mashindano hayo.

Mapema leo hakusita kuweka wazi juu ya Ufalme wa Afande Sele ambapo alisema “Ni wazi katika swala hili sipingi ufalme wa Afande Sele kiukweli alistahili. Ila mashaka yangu ni ile top 5 yao, maana walisema kuna vigezo vya kushirkiana wasanii katika nyimbo. Sasa wakati Afande Sele anachukua alkuwa na wimbo kama Darubini kali na mtazamo, katika wimbo wa mtazamo mimi na Prof Jay tumo pia Ferooz alikuwa kwenye top 5 na wimbo wa Bosi na Starehe ambapo tena mimi na Prof Jay tumo. Je tunawezaje kukosa kwenye top 5?

Swala kama hilo nikaona ni wazi mambo yalipangwa ila jamii ijue kuwa Afande Sele alistahili kuwa mfalme.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment