Abdu Kiba atuma salamu zake kwa Diamond Platnumz.

Abdukiba

Abdu Kiba atuma salamu zake kwa Diamond Platnumz.

Kidela ni wimbo wa pamoja wa Ali Kiba na Abdu Kiba ambao ulifanya vyema na kumuweka vyema Abdu Kiba katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Kuelekea kwa tuzo za BET ambazo zitatolewa jumapili ya kesho kutwa ambapo msanii Diamond Platnumz ndiye msanii pekee kutoka Afrika Mashariki anaeshiriki katika tuzo hizo.

Mapema leo Abdu Kiba hakusita kuweka wazi mawazo yake ambapo alisema “Kwanza nampongeza yani nampa hongera pia namtakia kila la kheri katika safari yake. Pia aweze kushinda tuzo hiyo maana anapeperusha bendera ya Tanzania.”

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez