“Hata Chid Benz alisema Joh Makini anabebwa” Young Killer.

“Hata Chid Benz alisema Joh Makini anabebwa” Young Killer.

Kumekuwepo na hoja nyingi mara baada ya wimbo wa Sinaga Swaga utoke. Katika wimbo huu Young Killer ameongea mengi ila wengi wamekuwa wakiongelea sehemu ambayo Young Killer amemtaja Joh Makini.

Katika wimbo wake huo wa Sinaga Swaga Young Killer amerap “Siku hizi bongo sio hiphop ni kisingeli, wanasema Joh anabebwa mpaka nahisi ni ukweli”

Mapema leo hakusita kuweka wazi maana yake ambayo alikuwa anamaanisha ambapo Young Killer amesema “Kwanza ni katika kuwekana  sawa maana muziki wetu unaruhusu, lakini pia ngoma za hiphop ambazo zilikuwa na misingi zilikuwa chache.

Lakini mimi sijasema Joh anabebwa  ila ni kwamba watu wanasema, hata Chid Benz aliwahi kusema hivyo kuwa Joh anabebwa alivyotoka Sober House, hivyo mimi nimefikisha ujumbe wa watu ambao wamekuwa wakiongea chini chini.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment