“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu ya 10-9

“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu ya 10-9

Habari za asubuhi mdau nina jambo ningependa lipitie kwako kwenda kwa wasanii wenzangu, nimeona si uungwana kujua jambo kisha kukaa nalo moyoni wakati pengine waweza kusema ukawa sehemu ya utatuzi.

Ninaomba nizumgumze part 10 hadi 1

Part 10.
Mziki wetu ulikoanzia haukuwa biashara bali burudani na halitapingika waliotutangulia walifanya jitihada kubwa sana kuutangaza na kujikuta wamejizolea umaarufu mkubwa. Kwa jamii na kuwa na majina yaliowawezesha wengi wao kupata fursa tofauti na sanaa zilizoendesha maisha yao.

Ila tangu wazee wetu wa zamani kaka na dada zetu walipoingia kwenye mziki jambo la kwanza walilokuwa hawalijui walikuwa hawajui thamani yao hivyo ilisababisha kufanya kazi kijamaa kirafiki ki mizuka na kazi zao zikawa zikienda kimizuka na mihemko ambayo ndio chanzo cha migogoro mingi inayotokea leo hiii.

Kwa kujali thamani ya majina yao walisahau kujipa nguvu kwa kuweka mipaka ya kutawaliwa na waliojiita WADAU Na hapo ndipo msingi wa tatizo lenyewe

Part 9
Wadau walikuwa na nafasi ndogo sana ya kimaamuzi juu ya sanaa yetu ni aina gani ya mziki wa kuimba na uweje lakini kwenye kipengele cha ushauri tu na sio mamlaka ya walitakalo liwe… sasa wasanii wakaanza kuwapa nafasi ya nguvu ya ushawishi juu yao. Kwa miaka yote wazee wetu walikuwa wakirekod kwa msaada wa studio za TBC na hakimiliki zote zilikuwa chini ya TBC na wengine hadi leo hawana umiliki wa kazi zao na baada ya kuwa na pengo au mwanya kwa lugha ya kitaalamu fursa ndipo wakatokea wadau walioanzisha mziki wa kizazi kipya ambao ulipata nguvu kubwa sana kwa aina ya uwasilishaji mada na hii ilitokana na upya wa aina ya mziki ule na jitihada za waanzilishi wa harakati za kuuinua mziki wa kizazi kipya wakiuita bongo flavour.

Na wadau wenyewe ni clouds media group Mr RUGE MUTAHABA na JOSEPH KUSAGA. Heshima zangu nyingi ziende kwao na kila siku nikumbukapo kusali huwa nawaweka kwenye maombi maana wana mchango mkubwa saana kwenye mziki wa bongo flavour. Sasa kwa kipindi chote hicho mziki wa kizazi kipya ulikuwa sio idea mpya duniani bali kwa tanzania ndio kilikuwa kitu kipya hivyo lazima iliwalazimu wadau kuangalia wenzetu waliotutangulia wanaendeshaji miziki yao ndipo wakagundua kwa wenzetu kuna Rec label yaani managment ya msanii lakini utofauti wa rec label na managment ya kawaida ni kuwa rec label ilijikita zaidi kwenye uzalishaji wa kazi za sanaa yaani kuuza album au single na rec label ilikuwa haizalishi tu zao bali na kulitaftia soko hapo ndipo ziliibuka SMOOTH VIBE, BONGO REC, MJ REC, nk.

Itaendelea …..

Na mwisho kwenye part 1 ndio tutamtaja msanii huyu. Tufuate kwenye mitandao yetu ya kijamii hapo chini

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez