“Hivi msanii unakataaje usilipwe mirabaha” Mchiz Mox

mchizi_mox

“Hivi msanii unakataaje usilipwe mirabaha” Mchiz Mox

Swala la wasanii kutaka kulipwa mirabaha lilianza kuchukua nafasi tangu mwaka 2002 lakini mwaka 2015 ndio mwaka ambao lilisikika kwa kiasi kikubwa.

Mpaka sasa upo mvutano ambao unaendelea chini kwa chini kuhusu wengine kutaka walipwe na wengine kutaka wasilipwe. Mchizi Mox ni moja kati ya wasanii wachache ambao huwa hawafichi mitazamo yake, maana wasanii wengi huwa ni waoga katika kutoa mitazamo yao.

Akiongea na Team tizneez Mchiz Mox amesema “Hakuna msanii aliyesema nyimbo zichezwe bure, ila baadhi yao ndio wanataka wasilipwe. Ila ambacho nimekisikia ni kwamba wapo wasanii walioandika barua katika vituo vya radio ili kazi zao zichezwe bure. Hivi msanii unakataaje usilipwe mirabaha?

Napenda kuwashauri tu wasijisahau wasijipindue wasiangalie leo, ila watu wa dizaini hii sidhani kama wanaweza kuandika urithi wa mtoto wake.Kama hutaki kufanyika kwa hili ni sawa hutaki kuacha urithi kwa familia yako.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez