Afande Sele Hajakubaliana na mabadiliko ya muziki?

Afande-Sele-nzuri_full

Afande Sele Hajakubaliana na mabadiliko ya muziki?

Mfalme wa muziki rhymes Selemani Msindi ambaye pia ni baba wa watoto wa wawili Tundajema na Asantesana, ambaye tangu anaanza shughuli zake za muziki aliamua kuishi katika mji wa Morogoro.

Afande Sele ambaye alijipatia umaarufu kwa vibao vyake kama Mayowe,Mkuki moyoni pamoja na nyingine nyingi. Pia alikuwa msanii wa kwanza wa hiphop kujaza uwanja wa mpira wakati wa uzinduzi wa album yake ya MKUKI MOYONI mwaka 2002, tumbuizo hilo lilifanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

2003 -2004 Afande Sele alishinda taji la Mfalme wa rhymes ambapo taji hilo anashikilia mpaka leo hii.

Afande ni msanii anayesifika katika tungo nyingi zenye kujenga na kuelimisha jamii. Kupitia tungo zake amejiwekea heshima kubwa katika ramani ya muziki wa kizazi kipya. Licha ya kuendelea kufanya muziki mpaka sasa 2016 na kutoa vibao vingi na vizuri lakini bado hafanyi vizuri kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kuna mengi yanaedelea katika muziki wa kizazi kipya, moja kati ya yaliyomengi ni madiliko ya kimuziki ambayo ukichunguza hayana msingi. Lakini walio wengi wamekuwa wakiwaaminisha wachache kuwa muziki umebadilika.

Afande sele ni moja kati ya wasanii ambao hawajakubaliana na mabadiliko hayo ya kimuziki. Muziki sasa sio kama ule wa miaka ya nyuma yani ukitoa wimbo mzuri wala hauhitaji kuhangaika kufanya video isipokuwa audio pekee itafanya vizuri tu tena kwa wakati huo huo ukiwa unaandaa album.

Dini tumeletewa ni wimbo mzuri na ni wimbo uliokuwa umebeba ujumbe mzito ambapo kila mtu anapaswa kusikia na kuelewa, lakini wimbo huu ulikosa video hivyo haukuweza kufanya vizuri. Hivyo ni wazi kama Afande Sele anataka kuwepo na kufanya vizuri katika ramani ya muziki wa kizazi kipya lazima akubaliane na mabadiliko ya kimuziki.

Ni wiki kadhaa nyuma amaetangaza kuja na kazi yake nyingine, ni vyema ikaja na nguvu ya mabadiliko yalioko sasa kwenye muziki ili kufanya vyema.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez