Leo ni kumbukumbu ya kifo cha mwana hiphop Father Nelly

Leo ni kumbukumbu ya kifo cha mwana hiphop Father Nelly

Father Nelly ni moja ya msanii ambaye alichangia kukua na kuenea kwa hiphop ndani ya nchi lakini nje.

Ambapo jina lake halisi ni Nelson Chrizostom Buchard.

Na alifariki Dunia kwa kuchomwa visu 9 katika sehemu tofauti tofauti kwenye mwili wake akiwa nyumbani kwao Arusha.

Father Nelly alikuwa ni muasisi wa kundi la XPlastaz ambalo ndilo kundi pekee lililotoa msanii aliyeshiriki kwenye Kilinge (Cypher) katika Tuzo za BET (BET AWARDS) 2009.

Nini Dhambi na Ushanta ni nyimbo ambazo ziliweza kumpa heshima kubwa katika utamaduni wa HipHop marehemu Father Nelly.

Father Nelly alizaliwa tarehe 18/2/1976 na kufariki tarehe 29/3/2006.

Na mpaka sasa imepita miaka 12 bila Father Nelly kwenye muziki wa Hiphop.
Nasi ni wale watu ambao tunaheshimu na kutambua mchango wake katika utamaduni wa hiphop.

Na tusifadhaike maana “hata kufa ni kuishi, ilihali ni kuishi katika kifo”

 

Tazama hapa wimbo wake wa Nini Dhambi ambao ni wimbo wake maarufu zaidi