Zimbabwe ya Roma ni mfano halisi #TuzungumzeMuziki

Zimbabwe ya Roma ni mfano halisi #TuzungumzeMuziki

Kwa hakika uongo juu ya muziki wa hiphop yakuwa hauuzi na haupendwi na watu fulani kama wakina dada, wamama, wababa na hata jamii ya watoto ni mkubwa mno. Lakini tukitazama kwa undani hoja hii ambayo hutolewa na wale ambao wamejivika vyeo vya udau ilihali hawana ufahamu yakuwa hakuna muziki usiokuwa biashara kwa maana ya namna jinsi utakvyotengenezewa mazingira ya muziki fulani.

Licha ya uongo mbaya kuanza kuwa ukweli mzuri kwa wengi ambao hawajui kwa undani mengi yahusuyo muziki wamekuwa wakiendelea kuamini yakuwa hiphop haiuzi wala haipendwi.

Lakini kwenye matamasha mengi makubwa wasanii wa hiphop ndiyo hukamilisha shoo kuwa shoo hasa lakini ndiyo huongoza kushangiliwa sasa hapa kipimo chao wadau yakuwa hiphop haiuzi wala haipendwi ni kipi?

Katika wimbo wa Mchaka Mchaka wa Mr II Sugu akiwa na Stara Thomas amesema “Ni upuuzi kusema hiphop haiuzi” Tukija kwa upande wetu kama Tizneez Imekuwa ni ngumu kufumba vinywa vyetu juu ya swala la kusema ukweli kwa maana kweli inatuweka huru.

Si kweli kama hiphop haipendwi wala haiuzi bali mdau hana mapenzi muziki huo, hivyo anataka kile ambacho yeye anapenda na mashabiki nao wapende hicho. Lakini haifai kumuamini mdau mwenye kuhubiri hiphop haiuzi wala haipendwi maana tukirejea nyuma ya wakati inatuonyesha yakuwa hiphop ndiyo chanzo cha muziki huu wa uimbaji hapa Tanzania (Muziki wa kizazi kipya) Hivyo ni vyema mashabiki kufahamu yakuwa hakuna muziki usiokuwa biashara, na hiphop inauza na inapendwa tena kwa upana na katika watu wote.

Hata kwenye wimbo wa Vita wa Nash Mc akiwa na P The Mc, Nash Mc alisema (THT) Tanzania Hiphop Tunauza, tena kwa bei ya juu. Hii ni kutokana na mambo mengi ambayo wasanii wamekuwa wakiyazungumza vyema kwenye nyimbo nyingi.

Mfano bora ni wimbo wa Zimbambwe kiukweli ni wimbo ambao unamgusa kila mmoja katika jamiii yake. Na tumeona jinsi ya watu ambavyo wanauzungumzia kwenye sehemu nyingi zenye mikusanyiko ya watu wengi. #HiphopInauzaHiphopInapendwa

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa