“Zima kiki washa muziki” Amber Lulu

“Zima kiki washa muziki” Amber Lulu

Afanyaye jema msifu kwa jema lake. Ni wazi tumepata wasaa mwema wa kusikiliza wimbo ambao ameshirikishwa Amber lulu na msanii aliyechini ya mwamvuli wa hiphop Edu Boy.

Wimbo huo umebeba wasanii wengine kama Stamina, Chid Benz, na BillNas. Lakini huu ni mwingine tofauti na ule wa mwanzo ambapo alikuwa Billnas na Edu Boy.

Alichoimba Amber Lulu hakika imeonyesha amekuwa vyema kwenye muziki. Amber lulu katika wimbo huu amesimama katika verse ya tatu ambapo ameweza kusimama vyema mbele ya wakali wote walioko katika ngoma hii.

Jambo hili ni jema na ni furaha kwa Team tizneez kuona Amber Lulu anakomaa kimuziki. Ni wazi katika mfumo wa dunia kimuziki mara zote mtu aanzaye kufanya aina nyingine ya sanaa na kujiingiza katika muziki huwa ni ngumu kufanya vyema.

Ila tayari Amber Lulu ameweza kukueleweka kupitia katika wimbo huu. Na hata kuimba kile ambacho watu wanamchukulia ila yapasa ajue kuwa muziki sio kiki wala mambo ya ajabu. Ni vyema kuanza safari yake ya muziki upya na yenye kujenga kesho yenye hekima na heshima kimuziki.

Na pia yapasa ajue “”Ulimi wa mwadilifu ni fedha bora, moyo wa mwovu una thamani ndogo” Hakuna sababu za kuacha kusifu kile alichofanya katika wimbo wa Edu Boy. Pongezi kwa Edu Boy kwa maana ya kutengeneza wimbo mwingine mzuri zaidi. #TuzungumzeMuziki.

Ni vyema Amber Lulu kufanya muziki wa kweli ili kuomgeza thamani yake na hata kuweza kutumika na makampuni mbalimbali. Maana katika uhalisia makampuni humtumia msanii mwenye nidhamu zaidi ya kazi na hata nje ya kazi katika kulinda kampuni husika.

#ZimakikiWashaMuziki.