ZIGO REMIX KUHAMASISHA USHOGA?

Nianze kwa kuomba radhi, pengine ni uwezo wangu mdogo wa kufikiri ndio unaonifanya kuandika hiki ninachotaka kukiandika wakati huu, lakini lengo sio baya, ni zuri mno. Zama zile wahenga waliamini kuwa mgema akisifiwa basi kinachofuata ni kujaza maji katika tembo. Sidhani kama hicho ndicho kilichotokea kwa Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni aliamua kujiita Simba. Pengine hakukosea sana kujibatiza jina hilo lakini asipo angalia usimba wake utaingia dosari kwa vitu vidogo ambavyo asilimia kubwa ya mila na tamaduni zetu inavipinga kwa nguvu zote.

Simba huyu anastahili kusifiwa kwa uhodari wake wa kuwinda pesa na hata warembo. Lakini moyo wangu unakuwa na simanzi kila ninapofikiria ule msemo usemao “Ivumayo haidumu.” Diamond Platnumz ni msanii ambaye amejibidiisha sana katika kazi yake, ambayo aliamua kuachagua kwa hiyari yake, kazi ya kuburudisha na kukonga nyoyo za watu kwa kutumia sauti aliyojaaliwa na Muumba. Hakika hakukosea kuichagua kazi hii, kwa jinsi anavyiimudu kiasi chakubadilisha maisha yake na kumwezesha kuishi katika Pepo ndogo iliyo duniani. Kiukweli anastahili pongezi, na ni mfano bora kabisa wa kuigwa katika yale yote mazuri ayafanyayo.

Zigo Remix ni wimbo mpya wa msanii nguli katika miondoko ya Komesho Ambwene Yesaya (AY). AY ambaye kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa ni msanii wa Tanzania aliyewahi kushirikiana na wasanii wengi zaidi kutoka nje ya mipaka ya Tz. Katika Zigo gwiji huyu aliamua kumshirikisha kijana machachari kabisa ambaye anasumbua katika mziki ndani na nje ya mipaka ya Bongo. Diamond ambaye aliutendea haki wimbo huo na kuongeza radha kwa kiasi kikubwa mno. Hili ni jambo zuri kwao wote, lakini pia liongeza radha nyingine ya mziki kwa mashabiki.

Pamoja kuwa wimbo una vingi vya kusifia, kitu kimoja ambacho binafsi sijakipenda, naweza sema kuwa ni uhamasishajia ambao upo katika Ubeti wa Diamond, Hebu tufikirie ni vijana wangapi watakao tamani kufanya mapenzi kinyume na maumbile mara baada ya kusikia sifa zilizomwagiwa mchezo huo mchafu ambao mtu yoyote mwenye hofu ya Mungu ndani yake angeukemea vikali. Tukitumia nadharia ya kwamba wasanii ni kioo cha jamii. Sikuona sababu ya kuimba ule mstari unaosema “KITANDANI SODOMA” Hakuna mtu ambaye asiyefahamu maana ya msemo huu kuwa ni mapenzi yanayofanywa kinyume na maumbile. Au ndugu yetu alikuwa hajui maana ya msemo huu? Na kama alikuwa hajui AY nae mara baada ya kuusikia kwanini alikubali uendelee kuwepo? Nini kimejificha nyuma ya wimbo huu?

Ama Diamond alitumia msemo ule ili kukamilisha vina katika ubeti wake? Lakini kuna maneno mengi sana ambayo yangeweza kutumika katika ubeti ule na ujumbe uliokusudiwa ungefika bila utata wowote. Ninacho kifahamu hasa kwa wasanii wakubwa kama hawa huwa hawatoi wimbo bila kuwasikilisha baadhi ya watu wanaowaamini ili kupata maoni yao. Je watu wote waliouona hawakuona utata uliopo katika utenzi huo?

Kama unamtazamo au tafsiri nyingine ya msemo huu, changia mawazo yako hapo chini katika comments.

Instagram tizneez Facebook tizneez Twitter tizneez