Yupo ambaye ametuliza mbona hamkunena lolote juu ya kumbukumbu ya Albert Mangweair katika kifo chake? (Ulizo

 Yupo ambaye ametuliza mbona hamkunena lolote juu ya kumbukumbu ya Albert Mangweair katika kifo chake? (Ulizo)

Ni juzi tu ya 28.5.2019 ambapo msanii Albert Mangweair alikuwa anatimiza miaka 6 tangu kuanza maisha yake ya kifo. (Huzuni)

Na Tizneez hatukuandika lolote lile bali tulipenda zaidi kuwa wasomaji wa posti za wengi. (Eeh)

Na wengi ambao waliposti waliweka wazi hisia juu ya huzuni katika kumpoteza msanii huyu ambaye inaaminika ni zawadi kuu iliyowahi kutokea Tanzania. (Muziki)

Vipindi vya Radio na Runinga hakika kwa siku ile ya 28.5.2019 ilikuwa ni kuhusu Ngweair tu si kingine. (Uhalisia)

Haikutupa shida katika hama hama ya vituo vya Radio na Runinga kila baada ya muda, lengo kuu ni ilikuwa ni kutaka kujua zaidi kila mmoja ananena yepi. (Usikivu)

Lakini wengi ni kwamba angekuwepo Ngweair ingekuwa noma sana hakika muziki ungemchangamka kinoma. (Wasemavyo)

Lakini nyakati yuhai hakukuwa na sifa hizi, lakini mbona bado tunao wasanii wengi wenye uwezo imara je! tunawathamini? (Ulizo)

Tunaheshimu na tunajua uwezo wa Ngweair lakini wapo wasanii wengine ambao wana uwezo mkubwa tu na tunao sasa, kwanini hawapewi nafasi kubwa? (Ajabu)

Leo wanasema Ngweair angekuwepo angekuwa noma, amini twaambia hawa hawa wasemayo haya wala wasingefanya lolote katika upana wa muziki wake. (Kabisa)

Kwani sasa wanafanya nini kuhusu Joslin? au kuna lolote mnasikia kuhusu Noorah?, si wiki kadhaa nyuma Jose Mtambo alitoa wimbo je ikawaje? (Chekesho)

Kaka yetu Stopa pia ametoa wimbo je! nani anazungumza kwa upana?. Lakini nafasi kuu ni kwa upana wa kuzungumza yakuwa “Gigy Money kapata baba mpya wa mtoto wake” (Soni)

Hawakawii kunena yakuwa “Stopa sio Ngweair” kwani sisi hatujui ama? tunazungumza kwa upana wa kutoa nafasi stahiki juu ya muziki. (Iko hivyo)

Lakini midomo yao ni miyepesi mno kunena kwa ukubwa juu ya Sister Fey na Bwa mdogo wake yule wamekimbizana mtaani wakipigana na hapo kupewa upana wa mahojiano. (Upuuzi)

Sifu na nafasi ya matendo imekuwa kubwa mno kuliko muziki wenyewe. Tuna wasanii wengi mno ambao wana uwezo mkubwa. (Iko Wazi)

Mkisema Ngweair angekuwepo ingekuwa noma ni kutaka kutudanganya ilihali uhalisi tunajua kwa upana wake yakuwa unafikia wa udaku ni mkubwa kuliko muziki. (Kabisa)

Lakini twajua kabisa yakuwa “Mtembea peku hapendi ila hana viatu” (Ufahamu)

#MuzikiNiSisi