Young Killer usiaminishe watu uongo. (Soni)

Young Killer usiaminishe watu uongo. (Soni)

Kuna nyakati huwa tunacheka mno kuona msanii akitaka kuchukua sifa ambazo si zake tena akiwa ni mwenye kujiamini zaidi. (Chekesho)

Tena wakati wa danganyo kuu kutoka kwenye kinywa chake, moyo wake unajua ukweli uwapi tena kwa mapana. (Hakika)

Young Killer anasema kupitia kituo cha Runinga cha Wasafi yakuwa “Album yake itakayotoka hivi karibuni yote ni ya mapenzi.(Eeh)

Na nimeona yakuwa ni idea ambayo haijawahi kufanyika” (Ajabu)

Lakini katika uhalisia msanii wa kwanza wa hiphop kutoa album yenye ujazo wa tungo za mapenzi tupu ni Azma Mponda.

Ambapo album hiyo inaitwa ‘Love Stories’ ambayo ilikuwa chini ya utengenezaji wa Duke ndani ya MLab, lakini Rock Town, Hisia, Bokazy Ent na Zakery Records. (2014/15)

Hii ni kweli yenye kweli katika kweli haswa, na uhalisi hakuna ambacho hafahamu Young Killer lakini dhanio kuu ni kuwa “Katikati pamemchanganya amesahau chanzo” (Upuuzi)

Na angeeleza kweli tu yakuwa Azma ni msanii wa kwanza kutoa album ya namna hii wala isingeleta matata. Bali heshima ingekuwa juu yake. (Naam)

Lakini dharau imekuwa kubwa juu yake kutoka kwa wajuzi kwa maana ametaka kuonekana yeye ndiye chanzo ilihali si yeye. (Fedheha)

Ni wazi Young Killer ametaka ufahari wa kuonenakana ni mwenye tofauti na wasanii wengi wa hiphop katika leo yake. (Ndiyo)

Lakini tunapenda kumkumbusha daima yakuwa “Fahari mama wa ujinga” ni vyema kuwa mkweli na kuvua ufahari ambao wachache wenye fuatilio la muziki wanajua. (Ukweli)

Mwanzo ni mwanzo tu daima katikati haiwezi kubadili mwanzo. (Tafakari)

#MuzikiNiSisi