“Young Killer na Uongozi wake wote ni vipofu watadumbukia shimoni, maana kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake”

“Young Killer na Uongozi wake wote ni vipofu watadumbukia shimoni, maana kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake”

Waswahili husema “Mwenye pupa hadiriki kula tamu” lakini daima haraka haraka daima haina Baraka.

Hatuachi kusema wakati wote yakuwa Young Killer ni bora katika vijana wengi katika muziki wa hiphop, kuanzia uandishi, midondoko lakini hata kwenye matumbuizo yake.

Young Killer huenda akapata anguko la kimuziki kama tu hatokuwa makini na aina ya utoaji wake nyimbo.

Ni wazi katika mwezi mmoja ameweza kutoa nyimbo 2 ambapo wa kwanza ni Kama hujanileta na wa pili ni Toto Tundu.

Na ni wazi utoaji wimbo mwingine unahamisha mashabiki kuhama kutoka kwenda wimbo wa kwanza na kuja kwa wa pili. Na mara zote msanii atoapo wimbo kwa aina hii ni wazi huua wimbo wa kwanza.

Lakini wapo wasanii ambao hutoa nyimbo mbili katika muda mchache na kuua zote, na hapa ndipo msemo wa waswahili unapochukua maana yake “Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote”

Wimbo wa Toto Tundu ni wimbo ambao hakupaswa kuutoa maana wimbo wa Kama hujanileta ni wimbo ambao ulihitaji nafasi ili jamii iweze kuusikia Zaidi.

Hofu ya anguko la wimbo wa Hujanileta imesababisha kutoka kwa wimbo wa Toto Tundu lakini Young Killer na Uongozi wake wanapaswa kujua “Hofu haina msaada Zaidi ya kukuvuruga akili”

Kuna haja ya Young Killer kupata uongozi mzuri Zaidi na sio alionao, ambapo ni wazi ni uongozi ambao haujui kusoma ramani ya muziki na namna ya kuufanya wimbo uweze kuwa mkubwa katika jamii bila kutumia Media.

Ni vyema kujitafakari kabla hazikuja nyakati mbaya za anguko la muziki, siis tunaamini juu ya kipawa cha Young Killer hivyo akipata uongozi wenye kujitambua ni wazi atafika mbali Zaidi.

 

 

 

 

#TuzungumzeMuziki

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa