Yapasa kujitakari kwa upana wa maswali juu ya Fifi, Jr Junior, na Dullah kwenye Planet Bongo.

Yapasa kujitakari kwa upana wa maswali juu ya Fifi, Jr Junior, na Dullah kwenye Planet Bongo.

Ni wazi nyakati zote kweli utuweka huru, nasi twapenda kuwa huru kama kweli yenyewe ilivyo. (Uhalisi)

Na hatuachi kusema yakuwa Planet bongo ni mahala pazuri katika endelezo jema la muziki lakini Hiphop kwa upana wake. (Muziki)

Chukizo ni namna ya ambavyo watangazaji hawa kuvaa kivuli cha kuendeleza hiphop ilihali hawana ujuzi wa uwanja wa maswali juu ya hiphop na msanii husika. (Mada)

Si mara moja kuhoji msanii swali moja katika hali ya mchangio lakini swali hilo likiwa halina maana wala faida kwa msanii na muziki kwa ujumla. (Fedheha)

Jambo hili ni lenye kujirudia mara kwa mara kwao na leo imejirudia tena kwa Jcb.

Pale ambapo aliulizwa swala la yeye kubadilika na kufanya muziki wa trap kama wafanyavyo wasanii wengine.

Ambapo awali alijibu kuwa “Siwezi kubadilika” lakini changio la swali moja liliendelea kwa hali ya upana.

Hatimaye Jcb kusema “Mbona tunazungumza jambo hilo kwa dakika 10 nzima” (Jazba)

Ni wazi katika kweli alishabadilika na kuona mahojiano hayana maana. Na sio kwake tu hata kwetu, lakini kwa mashabiki na wapenzi wa hiphop. (Alama za nyakati)

Lakini katika kweli kuna mengi ya kuongea na Jcb ukitoa hoja yao dhaifu ya kutaka abadilike.

Uwanja wa maswali juu ya Jcb ni mkubwa mno, na katika uwazi huwezi sema unaupa nguvu utamaduni wa hiphop ilihali unashikilia hoja dhaifu ya msanii kubadilika.

Hivi msanii abadilike nini? ili iweje? Ni wazi watu hawa hawajui na hawajui kama hawajui yakuwa “Hakuna muziki usiokuwa biashara” Sasa Jcb abadilike katika upande upi? (Soni)

Lakini kwa maswali ya kidaku kama “Hivi unamsikiliza kweli Chin Bees” hivi swali hili lina msaada gani katika muziki wa Jcb au hiphop kwa ujumla?

Katika kweli yapasa wajitafakari katika upana wa maswali yenye chachu ya maendeleo na endelezo jema kwa msanii husika lakini hiphop.

Lakini nyakati zote mswahili hunena yakuwa “Uzuri wa godoro wa nje tu, kwa ndani mna pamba” (Ufahamu)

Ilihali mswahili hakuacha kunena tena kwa upana yakuwa “Zito huwa pesi, ukilichukua”

#TuzungumzeMuziki