“Yamoto Band jahazi kubwa lililozama kiwepesi majini”

“Yamoto Band jahazi kubwa lililozama kiwepesi majini”

Nani mpenda muziki wa kizazi kipya asiyejua burudani njema iliyokuwa inatoka kwa vijana wanne ambao ni Maromboso, Aslay, Beka na Enock ambao kwa pamoja walikuwa wanaunda Yamoto Band.

Yamoto Band katika muda mchache waliweza kufanikiwa kuteka uwanja wa muziki wa kizazi kipya kwa ngazi ya ndani ya nchi lakini nje ya nchi.

Jahazi la Yamoto Band lilihimili vyema upepo wa mwanzo katika muziki huu uliojaa kila aina ya uchafu. (Rushwa, na Fitna)

Ni wazi katika ile kweli yenye kweli ambayo ni chukizo kwa wengi  kuanzia ngazi ya mashabiki, wasanii, na wadau ambao hawataki kabisa kuona ukweli ukizunguzmwa bali kusifiana uongo ilihali uongo hauna maana yoyote mbele ya ukweli.

Kasi ya upepo iliweza kuvuruga na kulipoteza jahazi la Yamoto Band ambalo ni wazi halikuwa imara kwa mfumo ambao walikuwa wanaenda nao wakisahau kabisa kuwa haipasi kuishi kwa mazoea.

Tunapoazungumzia mabadiliko ya muziki ni wazi tunagusia katika ngazi zote, muziki wenyewe, uendeshwaji lakini hata maisha ya wasanii nje ya muziki wenyewe.

Jahazi lao kuhimili upepo ilikuwa ni kazi kubwa ya ziada ambayo ilihitaji maarifa ya ndani ya muziki na nje ya muziki. Wakati huu kila mmoja amekuwa akiongea lake katika kujaribu kuficha aibu ya anguko lao, lakini daima “Ukweli hujitenga na uongo”.

Ni wazi Yamoto Band imeanguka na kila mmoja anafanya jambo lake mwenyewe wakiwa chini ya menejimenti tofauti, lakini Aslay akiendelea kubaki kwa meneja Chambuso ambaye alikuwa nae tokea enzi za uhai wa Yamoto Band.

Upepo wa mamlaka ya pekee juu ya Said Fella ndiyo chanzo kikuu cha jahazi hili kuyuimbushwa na upepo na hatimaye kupoteza muelekeo. Hakuna mwingine wa kulaumu ndani ya ukweli bali maarifa ya Fella.

Itaendelea…

Follow Twitter @Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa