Wimbo wa Kaolewa ni kiwango cha Rostam kweli?

Wimbo wa Kaolewa ni kiwango cha Rostam kweli?

Kaolewa ni wimbo mpya wa Rostam kwa maana ya Roma na Stamina. Ambapo Riyama Ally, Atan na Magic ni wasabii shirikishwa wakati Bea akiwa ni mzalishaji toka Kili Recods.

Na tumekuwa miongoni mwa watu wa mwanzoni kabisa ambao tumetazama wimbo huu mara baada ya kutoka. Na tumerudi kutazama zaidi ya mara kumi katika usikivu mzuri mno.

Na swali kuu kwetu huu wimbo wa Kalokewa ni kiwango cha Rostam kweli?. Hatuwezi kusema ni wimbo mbaya, la! hasha haupo katika kiwango cha Rostam. (Uhalisia)

Awali katika muunganiko wao tulitegemea kuona tungo kubwa zenye upana, na tulisifu mbele ya wajuzi wengi.

Hakika sasa kunako elekea katika uelekeo wa Rostam unaleta maana halisi ya semi ya mswahili yakuwa “Usijifu shauri ya kesho, maana hujui kesho itazaa nini”

Hatimaye leo ya kesho imezaa “Kaolewa”. Na upana wa Roma na Stamina katika tungo ni mpana mno, sasa nini kinatokea? au ndo wameamua kufanya rap katuni?

Na kuna haja gani kila nyimbo wafanye katika mlengo wa majibizano? Hapana ni wazi itaboa hasa katika tungo nyepesi za namna hii. Sahau kuhusu Now You Know na Kaligraph.

Bado imani yetu ni kubwa katika upana wa Rostam, na tunaamini kabisa watapiga madude yenye upana mkubwa si kama ‘Kaolewa’ au ‘Kibamia’.

Kuna hofu yoyote juu yao yakuwa tungo nzito zitakuwa si biashara?. Huenda lakini wanapaswa kujua yakuwa “hakuna muziki usiokuwa biashara” (Kweli)

Hivyo hata wakiachana kufanya rap katuni na wakasimamia simamio la ujazo wa tungo zao hakika watapata matokeo makubwa zaidi.

Kikubwa ni kuweza kutangaza kazi zao kama ambavyo wanatangaza hizi sasa kama Hivi Ama Vile, Kibamia, Paranda na sasa Kaolewa.

Na daima mswahili hunena yakuwa “Tunapaswa kubadilika kulingana na mazingira, ila si kila mazingira yatubadilishe”.

Biashara ya muziki na muziki biashara ni changanyo kwao, na wala msiyumbe maana “Hakuna muziki usiokuwa biashara”

#TuzungumzeMuziki