“Weusi wanastahili pongezi kwenye tamasha la Castle Lite Unlock”

“Weusi wanastahili pongezi kwenye tamasha la Castle Lite Unlock”

“Daima shahidi ndiye mwenye neno” na hatuachi kutoa ushahidi mbele ya wapenda muziki waliowengi ambao hawakuweza kufika siku ya Jumamosi ya tarehe 22/7/2017 katika viwanja vya leaderz Club kwenye tamasha la Castle Lite Unlock.

Castle Lite Unlock ni moja kati ya tamasha ambalo lilikuwa na wasanii wachache mno. Na kila msanii/wasanii alikuwa/walikuwa na uwezo wake/wao binafsi ambao kila shabiki aliyeudhulia eneo lile shauku ya kuwaona/kuona tumbuizo la msanii husika ilikuwa kubwa.

Weusi ndiyo walikuwa vinara wa kufungua tamasha lile katika ile ya listi ya wasanii husika ambapo ikumbukwe tamasha hili lilikuwa likiwahuisha NavyKenzo, Cassper Nyovest, Future, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee.

Aina ya kujipanga kwa Weusi ilifanya wawe bora katika wasanii wote wa nyumbani ambao walituwakilisha katika tamasha hili.

Upangiliaji wa nyimbo, kujua kucheza na mashabiki, uchaguzi sahihi wa nyimbo za shoo, hakika mambo hayo yalifanya wawe bora na kuweza kuteka hisia za kila mmoja aliyewekuwepo kwenye uwanja ule. Ikumbukwe sio nyimbo zote hufaa kwenye tamasha na Weusi walijua hilo.

Ila jambo pekee ambalo liliendelea kuwafanya mashabiki wafurahie shoo ya Weusi ni namna kupiga nyimbo kwa ufupi mno kama sio chorus pekee, lakini mtindo wa kupeana nafasi ya kati ya Gnako, Nikki, na Joh Makini

Hakika katika matamasha mengi tunaona wasanii wengi wakilazimisha kuimba nyimbo nzima ilihali katika uhalisia ni ngumu mshabiki kuimba na msanii mwanzo wa nyimbo mpaka mwisho, ila ni rahisi shabiki kuimba chorus tu na nusu verse kwa ufupi.

Ujanja wa kusoma mchezo unavyokwenda Weusi waliweza kufanya vyema kuliko msanii yoyote kutoka nyumbani. Jambo hili likuwa ni ngumu kwetu kufumba vinywa vyetu katika kuwapa pongezi hizi Weusi kwa maana ya Nikk wa pili, Gnako, na Joh Makini.

#ZimaKikiWashaMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa