Weusi wamejua yote kufanya muziki na kuufanya biashara

Weusi wamejua yote kufanya muziki na kuufanya biashara.

Kujua muziki kwa kuufanya ni kitu mosi, lakini pili ni kuufanya uwe biashara kwa wengi kwa maana ya kuutafutia soko kwa mapana.

Na changamoto kwa wasanii wengi kujua namna ya umbili mara mbili kwa maana kufanya muziki na kuufanya biashara.

Na daima ili muziki uwe biashara ni lazima uwape watu kile wanataka na usifanye kile utakacho wewe. (Uhalisi)

Weusi kwa Swagiree naam! hatuna cha kunena zaidi ya mmekwiza katika upana wa kujua soko liwapi hivyo ni katika ukamilisho wa bidhaa yenye uhitaji kwa nyakati kamili.

Mitambao yenye ladha ya wepesi katika kushikika ni njia kubwa ya wimbo kufanya vyema katika soko.

Lakini kwa namna mlivyopita mmepita vyema kila mtu na ladha yake ambayo haichoshi na tofauti tangu na tangu Weusi ianze.

Hakika nafsi za Weusi zimejaa njaa ya kushika soko kwa upana wa sanaa ya muziki wenye ukamilisho. Na njaa hiyo isiishe kwa maana “nafsi yenye njaa huona kila kitu kitamu”

Basi fanyeni kwa upana wa njaa ya muziki katika kile ambacho soko linahitaji na wala msiyumbishwe na mengine bali tazamo la muziki kwa upana wa soko.

Pongezi kwa S2kizzy kwa namna yake amefanya kazi nzuri yenye uzito wa kwenda na upana wa uhitaji wa soko.
Naam! #TuzungumzeMuziki