Weusi si hiphop kwa kanuni zipi? (Ulizo)

Weusi si hiphop kwa kanuni zipi? (Ulizo)

Mjadala wa Weusi si hiphop ni mpana kwenye makundi mengi ya Hiphop katika mtandao wa ‘WhatsApp’ wamekuwa na jadilio kubwa. (Ndiyo)

Na shangazo kubwa ni shambulizi nyingi yakuwa Weusi si hiphop kabisa. Na semi za lugha kali hutawala mno katika semi zao. (Ajabu)

Lakini je! ambao wananena Weusi sio hiphop wanatumia kanuni zipi? (Ulizo). Maana ni vyema tujadili kwa uwazi na kanuni zenye uhalisi katika kujenga. (Eeh)

Sasa Weusi sio hiphop kwa kanuni zipi au kanuni ipi? (Tujuze). Maana katika kweli yenye kweli ni wazi Hiphop ni utamaduni kwa ujumla wake. (Kabisa)

Kama Hiphop ni utamaduni mnawezaje kusema Weusi sio Hiphop?. Je! Utamaduni wa Hiphop unakataza msanii/wasanii kufanya aina nyingine ya muziki? (Wapi)

Changamoto iliyoko kwa watu wengi ndani ya tamaduni ya hiphop ni kukariri na kujifungia katika kichumba kidogo cha tafakari. (Kweli)

Wao hudhani mwenye kutumia mdundo wa bumbap ndiyo hiphop. (Sio kweli). Hiphop ni utamaduni na daima hakuna mahala ambapo msanii anaweza kukatazawa kutumia mdundo mwinginie na akitumia sio hiphop. (Hapana)

Hivyo ni vyema ndugu zetu wa (Ipapu) mjue yakuwa hakuna katazo la msanii/wasanii kufanya wimbo katika mdundo tofauti na bumbap. (Kabisa)

Kikubwa ni kuweza kuishi vyema ndani ya mdundo huo na kuweza kuwakilisha kile alichonacho katika wimbo husika kwa uhakika (Naam)

Je! bado mnaamini Weusi sio hiphop? ni wazi tuache wasanii hawa wafanye ambacho wanaweza katika ukubwa wa vipawa vyao, muda wa kujadili huyu ndiye huyo siye hauna maana bali muziki kamili utaishi. (Kwa uhakika)

Ni wazi “Kumpangia msanii cha kufanya ni kuweka mipaka katika kipawa chake” (Tuache)

Weusi ni hiphop sisi tumenena kwa uhakika, maana hakuna kanuni ya kufanya kuwaona sio hiphop. (Kabisa)

#MuzikiNiSisi