Wenye kujua maana ‘Biashara’ hakika watampongeza Ali Kiba.

Wenye kujua maana ‘Biashara’ hakika watampongeza Ali Kiba.

Tupo katika kizazi cha ujuaji ilihali hakipendi kutafakari katika upana, ila hisia huwaendesha kwa namna ya upana. (Soni)

Na hakika kundi wa wakosoaji ni kubwa ilihali kukosoa bila kujua uhalisi kwa hakika umepotoka vyema. Ali Kiba ametanua wigo wa biashara yake ya muziki katika upana wa biashara ya kinywaji ambacho kinaitwa ‘Mofaya’.

Ambapo 29.4.2018 alitangaza rasmi yakuwa ni kinywaji chake, ambacho hivi karibuni kitaanza kupatikana katika kila mtaa. Na tayari tunaona baadhi ya watu wakitumia nguvu kubwa katika kusema yakuwa “Si chake, na wala hana uwezo wa kuwa mmiliki”

Jambo hili linatufanya tutumie kalamu zetu vyema katika usahisho wa watu wenye fikra nyepesi na rahisi mithili ya urahisi wa mtu afunguapo taulo msalani.

Kabla ya dhihaka juu ya Ali Kiba, Kwanza walipaswa kutafakari neno ‘Biashara, ambapo Biashara ni Muuzo wa kitu au huduma katika muundo kwa wateja ambacho hutambuliwa kisheria katika uuzo kwa jamii (Wateja) na lengo likiwa ni katika mfumo wa kuongeza pato kwa mhusika.

Lakini biashara inaweza kumilikiwa na mtu binafsi au watu Zaidi ya wawili au Zaidi na Zaidi (Umiliki). Na katika uhalisia sio wafanyabiashara wote wenye kumiliki bidhaa kadhaa basi wao ndiyo waanzilishi, hapana. Hivyo ni shangazo kushangaa uwepo wa “Mofaya” kabla ya Ali Kiba kutangaza kuwa ni ya yeye.

Ni vyema kujua yakuwa wapo ambao hununua biashara yote katika umiliki  wa pekee au watu zaidi ya mmoja na kuongeza jina au kubadili jina au katika hali ya kuacha jina kama lilivyo, yote yanawezakana katika mlengo wa hitaji lake na mlengo wake mhusika kibiashara.

Hivyo katika yote yafaa kabla ya ukosoaji na udharau ni vyema walio wengi wajifunze katika mlengo wa kuwaza katika mfumo wa uelewesho.

Hakika sisi tunajua maana ya upana wa neno biashara hivyo hatuachi kusema pongezi kwa Ali Kiba kwa hatua hii kubwa.

Picha ya Kinywaji cha Mofaya

#TuzungumzeMuziki