“Watu walianza kutatua tatizo ndiyo wakapata fedha, na sio kupata fedha kutatua tatizo” Young Killer

“Watu walianza kutatua tatizo ndiyo wakapata fedha, na sio kupata fedha kutatua tatizo” Young Killer.

Tukikumbuka kumbukumbu ni mnamo tarehe 19.12.2017 tuliandika andiko hili yakuwa

“Young Killer na Uongozi wake wote ni vipofu watadumbukia shimoni, maana kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake”

Na kweli hii iliwaumiza genge lake lakini msanii mwenyewe na kuamua kuufunga mtandao wa Tizneez katika mtandao wa picha ‘Instagram’

Ila katika uhalisi tuliandika kwa maana ya kuweza kumfanya atafakari katika upana wa kubadilisha genge ambalo lilivijika usimamizi wa kazi ilihali hawajui usimamizi wala maana ya usimamizi.

Katika kweli yenye kweli hatuachi kusema upana wa kipawa cha Young Killer ni mkubwa mno, hivyo hakuna kingine ambacho anahitaji zaidi ya usimamizi imara wa kazi zake.

Ni wazi Young Killer hakuwa anajua yakuwa “Watu walianza kutatua tatizo ndiyo wakapata fedha, na sio kupata fedha kutatua tatizo”

Hakika alichokuwa anakifanya wakati yuko katika genge lisilojua maana ya biashara ya muziki ni kupata fedha kutatua tatizo na sio kutatua tatizo ili kupata fedha. (Ufahamu)

Maana hawakuwa watu wenye mtazamo wenye maendeleo bali kuwaza mawazo madogo ya leo yenye leo sio kesho yenye kesho ya ukubwa.

Hakika Young Killer kuangikia katika mikono ya Wanene Studio kwa hakika sasa yu katika mikono salama na nyeye utambuzi wa biashara ya muziki.

Team Tizneez tunakupongeza kwa hatua hiyo ya kujiunga Wanene na tunaamina, nidhamu ya kazi itakuwepo kwa hali ya juu huku mafanikio yakikufuata.

Pongezi zetu ziwe nawe.

#TuzungumzeMuziki