Watu wa Mwanza Je! Mnajua hakuna Awali mbovu?

Watu wa Mwanza Je! Mnajua hakuna Awali mbovu?

Mpewe nini katika ujazo wa burudani yenye aina tofauti ya ladha ya muziki?

Tukitafakari kwa upana wa orodha ya wasanii ambao leo watakuwa kwenye tamasha la “In Love & Money” hakika hatuoni sababu ya watu wa Mwanza na maeneo ya karibu kushindwa kufika.

Na Mwanza mmekuwa ni wenye bahati ilioje!!! kwa kuwa watu wa kwanza kukata utepe wa tamasha hili.

Hakika ni upendo, na mswahili hunena yakuwa “Apewae mwanzo ndiye mwenye thamani”

Hivyo thamani yenu ni kubwa maana Jux, Vannesa, Gnako, Nikki wa pili, Joh Makini, Mimi Mars na wengine wengi wamewapa nyinyi burudani ya kwanza katika “In Love & Money”.

Hivyo ni vyema jioni ya leo kufika kwa wingi katika eneo la Rocky City Mall ili kuweza kupokea utamu na ladha ya muziki.

Na ukarimu wenu Mwanza tunajua mnajua thamani ya mtu kukupa uthamani wa mwanzo, Naama twaamini leo mtapokea zawadi yenu ya burudani kwa hali ya upana, wingi na utulivu.

#TuzungumzeMuziki