Watu wa ‘Media’ hamuoni soni mbele ya Domokaya?.

Watu wa ‘Media’ hamuoni soni mbele ya Domokaya?.

Ni nini hasa kimewapa upofu katika muziki kamili wa Domokaya? Pesa, kiki, au nini labda?. Mbona hamuoni hata soni?

Maana nyakati zote sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa, hivyo hata moyo wake hupata maarifa.

Nyinyi masikio yenu yanatafuta hasa nini? lakini mnataka watu wasikie nini zaidi kutoka kwenu?.

Na hii katika uhalisi mpana, maana wenye kujua uraha wa muziki daima huutafuta vyema, lakini wasiojua wao hutafuta matendo zaidi. (Kiki)

Mbona nanyi mmekuwa ni wenye kuhubiri zaidi mengi ya hovyo? (Kiki). Ni nani aliyewaroga na kuwalaghai yakuwa ‘kiki’ itapandisha muziki?.

Daima ‘kiki’ haiwezi kupandisha muziki hata iweje katika ile kweli, bali muziki wenyewe wenye ujazo kamili wa muziki.

Lakini nani anajali hilo? hakika hakuna. Maana hata watu wa ‘Media’ ni wapenda zaidi hovyo za kiki si muziki. (Chekesho)

Kwani hatuoni? upana wa mengi ya hovyo yapewavyo muda wa kutosha katika vipindi vya Radio na Runinga?

Na wenye ya hovyo muziki wao uko wapi? hakika ni juu, lakini wenye muziki kamili ambao hauna hovyo je! muziki wao uwapi? Naam! kapuni. (Soni)

Katika kweli yenye kweli ni ‘Media’ ipi kwa upana Radio na Runinga ambayo walau mmesikia habari njema za kanda mseto ya Domokaya au hata wimbo tu wa ‘Mcheza kwao’?.

Nani anajali muziki mpaka umsikie Domokya? zaidi ya kuona amepitwa na nyakati maana hatendi ya hovyo bali muziki. (Upumbavu).

Ni wazi kanda mseto ya Domokaya ipo na ukamili wa hali ya juu na hakika anapaswa kupewa nafasi kwa upana wake.

Kukaa kimya juu yake ni jambo lenye ujazo wa soni kwa ‘Media’ tena kila siku ni wenye kuigana vyema katika ‘maudhui’ yenye kiki. (Fedheha).

Hebu mtazameni Domokaya katika upana wa kazi yake ya sasa, kumpa kisogo ni kumkosea yeye na mashabiki wengi wenye kupenda muziki.

#TuzungumzeMuziki