Watayarishaji chipukizi kipo cha kujifunza juu ya Lamar.

Watayarishaji chipukizi kipo cha kujifunza juu ya Lamar.

Kujifunza ni jambo jema ambalo linaweza kukupa mabadiliko ya maisha yako nyakati zote.

Lakini ukiwa si mtu wa kujifunza kila leo ni wazi utaambulia hasara kila leo.

Na nyakati zote waswahili hutukumbusha yakuwa “ Shika lenye maana maana litakupa maana”

Huwezi kutaja watayarishaji bora wa muda wote bila kutaja jina la lamar. Ni wazi kwa nyakati zake aliweza fanya mema kwenye huu muziki.

Wimbo kama Mimi wa Geez Mabovu, Pompo pisha ya Chid Benz, Moyo wangu ya Diamond Platnumz, na nyingine kwa ukubwa wake zilinogesha na kuupaka wanja muziki huu.

Hakika Fishcrab ilikuwa ni nyumba ya nyimbo bora za wakati wote.

Ila kazi aliyofanya ni wazi haikuweza kumlipa vyema kulingana na wasanii husika vile wanaendesha muziki.

Leo hii hatumsikii Lamar katika utengenezaji muziki bali tunamuona katika biashara ya uoshaji magari.

Si jambo baya maana yote ya yote mkono uende kinywani. Ila ubaya ni sisi kumkosa Lamar kwenye uwanja wa muziki huu ambao ni wazi bado tunahitaji kumsikia vyema na kuendela kuupaka wanja muziki huu kwa viganya vyake vye ladha tofauti na wengi.

Lakini atarudi vipi wakati wasanii si watu wa kulipa kwa mtayartishaji? Hivyo yapasa ang’ang’ane kwenye uoshaji magari ilihali ilihali ilipaswa ule uwe uwekaji huku akiendelea na utayarishaji muziki wakati biashara yake hiyo ikiwa yaendelea.

Nasi twampongeza kwa uwekezaji huo wa uoshaji magari, lakini hatuachi kuwaambia watayarishaji ni vyema wajifunze juu ya Lamar maana wasanii hawana soni mara baada ya mafanikio yao.

Ni vyema kuchukua tahadhari mapema katika kujikomboa kiuchumu maana nyakati hazirudi nyuma.

Na tunaona namna ya wasanii wakubwa wanavyowakimbilia watayarishaji wachanga si kana kwamba ni bora bali hutaka bure Zaidi.

Ni vyema kujua kuwa “Maji huteremka bondeni hayapandi mlima”

Tafakari…!!!!

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa