Watangazaji na madj wengi hawasapoti muziki wa hiphop bali msanii.

Ni vyema tuijue tofauti ili kweli ionakane kwa mashabiki.

Watangazaji na madj wengi wamekuwa wakivijika vazi la kusapoti muziki wa hiphop ilihali wengi wao ni waongo.

Kwanza lazima tujue yakuwa “Kuna kusapoti muziki wa hiphop na kuna kusapoti msanii wa muziki wa hiphop”

Wengi wanasapoti msanii wa hiphop na si muziki wa hiphop, na wengi nyuma ya pazia huwabania wale ambao ni wazi kama wangepewa nafasi ndogo tu ni wazi tungeona ukubwa wa vipawa vyao kwenye muziki huu wa hiphop.

Ya nini watangazaji mhubiri uongo yakuwa mnasapoti muziki wa hiphop ilihali ni msanii wa hiphop?
Na tukitazama kwa mapana msanii husika hafai kutajwa kama yumo kwenye kundi la hiphop bali mhangaikaji asiyejua upana wa muziki husika.

Hakika yafaa muwe wa kweli kwa kusapoti muziki wa hiphop kwa ujumla na si msanii au wasanii kadhaa.

Kuvijivika vazi la kusapoti hiphop ilihali si kweli ni jambo baya.

Hatuachi kumpongeza mtu kama Ezden The Rocker na Dee 7 moja ya watu watangazaji ambao walisapoti muziki wa hiphop na si msanii wa hiphop, nyakati hizo za Kiss Fm Mwanza.
Ni nani msanii wa hiphop na shabiki asiyejua haya ya nyakati za Kiss Fm? Na aseme hadharani kama si kweli haya tuyanenayo.

Lakini hatuwezi kumsahau Dj Mafuvu kwa nyakati zake hakika alikuwa ni mwenye kusapoti muziki wa hiphop si msanii.( Ea Radio)

Bila kificho haitupi tabu kusema yakuwa yafaa wenye kuhubiri wanasapoti muziki wa hiphop waende sawa na neno hilo, isiwe kusapoti msanii na useme unasapoti muziki wa hiphop.

Ni vyema kujua kutofautisha ili uweze kupata tofauti yenye kujenga leo zetu na kesho zenye usawa wa maisha ya muziki wa hiphop.

Na ni vyema kuacha kujivika vazi ambalo ni wazi linakupwaya, huku ukiaminisha watu yakuwa ni hivi kumbe ni vile. (Fedheha)

Na ndugu zetu watangazaji na madj andiko hili halipaswi liwe chukizo kwenu maana mswahili hunena kwa semi ya yakuwa “Kupoteya njia ndiyo kujua njia”

Tafakarii….!!!!!

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment