Watangazaji chanzo cha dharau kwa wakongwe wa bongo fleva/hiphop Sehemu ya I

radio-mic-high-res-1000x500

Watangazaji chanzo cha dharau kwa wakongwe wa bongo fleva/hiphop Sehemu ya I

Inatosha kuona nadhani bora kusema, sanaa ni kioo cha jamii toka awali. Kwangu ni furaha kuona kila siku muziki wa kizazi kipya unakuwa kila iitwapo leo. Napenda kusahihishwa na sio kulinganishwa”haya alisema Prof Jay katika wimbo wake wa Sauti ya Gheto.

Inaweza kukupa tabu kidogo juu ya kusema “Watangazaji”ila hapa nina maanisha juu ya watangazaji wa vipindi vya burudani hususani muziki wa kizazi kipya, wa pande zote mbili kati ya Radio na Runinga.

Hakika kama umetimia katika kichwa chako hutaacha kusifia wakongwe wa muziki wa muziki wa kizazi kipya vile ambavyo wamepambana kukuza na kueneza Muziki wa kizazi kipya. Maana wakati wanapambana hakukuwa na vituo vingi vya radio na Runinga kama ilivyo sasa. Sugu aliwahi kusema “Kama hupigi nyimbo zangu radioni hamna maneno,Mimi nimenza kurap kabla ya fm” alisema hayo katika wimbo wake Moto chini.

Historia inatuonyesha mtangazaji wa kwanza kupiga muziki huu radioni alikuwa ni Taji Liundi katika miaka ya 1994 katika kipindi cha DJ Show  katika kituo cha Radio One. Ambaye sasa sina hakika yupo katika kituo gani, maana mengi yametokea hapa katikati.

Hakuna jambo jema kama kukumbushana yaliyomema yenye tija katika jamii yetu,  ambayo ni wazi sasa imetekwa na muziki huu wa kizazi kipya. Muziki huu leo hii umegeuka lulu lakini ikumbukwe zamani miaka ya 1992 ulikuwa ukionekana ni uhuni.

Nichukue nafasi hii kuwapongeza wasanii wote ambao walichangia muziki hadi kufika hapa ulipofika. Kutoka katika uvungu wa moyo wangu nawapongeza sana hakika mmefanya kazi kubwa kueneza na kukuza muziki huu, ambapo leo hii umekuwa mkubwa kiasi katika vituo vya radio na runinga vilivyo vingi 99% ya vipindi vya vinaongozwa na nyimbo kama sio mahojiano ya wasanii wa kizazi kipya.

Si mara moja wala mbili kusikia mtangazaji wa Radio au Runinga akimlinganisha msanii mkongwe na msanii wa sasa. Tena bila kuona aibu husema wazi “wee jamaa mkali kuliko yule” au mtangazaji kusema maneno yasiyofaa juu ya msanii mkongwe. Ni miaka kadhaa imepita pale ambapo mpiga miluzi hodari wa kike ambaye sasa sina hakika anafanya shughuli gani alipoamua kuzungumza kauli zisizofaa juu ya msanii mkongwe Afande Sele, tena akiwa katika muda wa kipindi. Na hata kumlinganisha na msanii zilla na mfalme Afande sele, mpaka leo nimekuwa nikijiuliza je alikuwa analinganisha katika upande gani? Hivi ufahamu wake upo sawa? Au hajui kama kuna tofauti kubwa kati ya maji na maziwa?

Inafika wakati ni vyema kukumbushana majukumu yetu, ambayo ni wazi huwa sifa zinawalesha walio wengi. Si jambo baya kuambiana ukweli, isipokuwa ni jambo baya kusifiana uongo.

Imekuwa ni mila na desturi sasa hata watangazaji kutosema…. Itaendeleaa

Tufuate Twitter Tizneez Facebook Page Tizneez Instgram Tizneez Youtube Tizneez