Wasanii wenye malalamiko na Media ni vyema Best Nasso akawa somo.

Wasanii wenye malalamiko na Media ni vyema Best Nasso akawa somo.

Tukizungumza kweli yenye kweli, hivi tukitoa Tbc ni Radio/Runinga ipi ambazo zimewahi kucheza nyimbo za Best Nasso kwa upana lakini hata kuwepo katika top 10 au 20 Jijini Dar es salaam?

Ni wazi hakuna kabisa, lakini Best Nasso anabaki kuwa msanii pekee mwenye shoo nyingi mikoani.

Na katika uhalisi Media za mikoani zinacheza kwa hali ya juu nyimbo zake na hata kuweza kushika namba za juu kwenye chati mbalimbali za muziki.

Na kushikana vyema na radio/runinga za mikoani amekuwa akifanikiwa vyema kwenye muziki wake.

Mfano hai ni mwaka 2017 tulikuwa Mwanza, Wilaya ya Ukerewe kisiwani Ukala na kukuta shoo ya Best Naso.

Na aliweza kujaza kwa hali ya ukubwa, na wahusika kusema “Hii ni mara yake ya tatu kuja hapa na hakuna msanii yoyote aliyewahi kufika hapa ukala”

Lakini pia mwaka 2016 Mtwara pia tuliambiwa na wadau kuwa ni mwenye kufanya shoo nyingi, ilihali mwaka 2017 hata Kasulu Kigoma pia alifika.

Katika kweli sijui uende upande gani wa Tanzania na ukute Best Nasso hajafika kufanya shoo.

Lakini je!ni kituo gani cha Runinga au Radio kinachompa nafasi Best Nasso hapa Dar es salaam?

Hivyo ni vyema msanii kuamka kifikra na kuvua mawazo ya kubaniwa na Media za Dar es salaam bali kwenda katika ngazi ya mikoa zaidi.

Tanzania ni kubwa ndugu zetu wasanii, na mashabiki wenu wapo kila upande hivyo ni vyema kuchangamsha akili.

#TuzungumzeMuziki