Wasanii wenye malalamiko hamna cha kujifunza mbele ya wasanii wasio na malalamiko

Wasanii wenye malalamiko hamna cha kujifunza mbele ya wasanii wasio na malalamiko?

Wapo wasanii wengi mno ambao wao kutwa kucha ni malalamiko kuwa anabaniwa na Media. (Fedheha)

Lakini malalamiko yamewahi kutatua tatizo? (Hapana) bali kuliongeza kwa upana wa chuki kubwa kati ya msanii na Media. (Ndiyo)

Na hatuachi kuweka kumbusho yakuwa “Biashara ni mahusiano” la! hasha “Biashara ni matangazo” (Uhalisia)

Kama umeona hapa wanabana na huna mahusiano mazuri tengeneza njia ya mahusiano na wengine, lakini jitihada za kuweka usawa wa mahusiano ziwepo. (Kote)

Na semi yenye uhalisi wa uhalisia wa mswahili ni “Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako”. (Naam)

Vivyo basi kabla hujaanza kulaum yakuwa Media fulani inabana, wewe kama wewe msanii umetumia ukurasa wako wa mtandao wa kijamii katika kutangaza kazi yako kwa upana? (Ulizo)

Sasa kama msanii hujaweza kutumia mtandao  katika ukurasa wako kutangaza biashara yako kwanini ulaum watu wengine? (Ajabu)

Pia ikumbukwe nyimbo zimekuwa nyingi mno na matangazo pia yamekuwa mengi, hivyo usitaraji wimbo wako kuchezwa kwa uzima kwenye kipindi. (Hakika)

Vipindi vingi hucheza wimbo nusu tu kulingana na muda wao kuwa mdogo zaidi.  Vivyo wasanii wenye lawama msilaum kupita kiasi bali tazameni uhalisi. (Nyakati)

Tumeona mwezi wa huu wa kwanza kumetoka nyimbo nyingi mno na ni kutoka kwa wasanii ambao ni listi ya kwanza kwenye bongo fleva/hiphop. (Ndiyo)

Je! wasanii wenye malalamiko mmeona

wasanii hawa wanavyohangaika katika kutangaza kazi zao kwenye ngazi ya mtandao? (Ulizo)

Sasa inashangaza kuona wasanii wengine wametoa wimbo/nyimbo lakini kutwa yeye ni lawama tu katika wengine. (Ajabu)

Muda ambao unatumia kulalama ni vyema ukatangaza biashara yako kwa ukubwa, lawama haziwezi kuwa msaada bali fedheha juu ya wewe/wao. (Kabisa)

Pongezi kwa wasanii wote ambao mtandao umekuwa ni ngazi ya kutangaza kazi zao si malalamiko yasiyo na maana wala maana. (Pongezi)

#MuzikiNiSisi