WASANII WENGI WA BONGO BADO CHIPUKIZI KWA KUKOSA ALBUM

cdcover_standard_psd_165065

WASANII WENGI WA BONGO BADO CHIPUKIZI KWA KUKOSA ALBUM

“Msanii chipukizi” kwanza kabisa neno chipukizi ni neno lililotokana na neno chipukia hivyo asili ya neno chipukizi ni neno chipukia. Wakati neno hilo chipukia lilikuwa na maana ya kuchomoza yani kuanza kuonekana tokea chini, maana hii inaweza kuwa kuchomoza katika kitu chochote kile. Hivyo msanii chipukizi ni msanii ambaye ameanza kuonesha wazi uwezo wake wa kisanaa, pia nia kuu ya msanii chipukizi ni kuhitaji akili za watu au wapenda sanaa ya muziki kuangalia na kujadili kazi yake ya sanaa. Msanii chipukizi kwa lugha ya kigeni (English) ni Upcoming Artist

Muziki wa kizazi kipya ambao ulianza kushika hatamu miaka ya 1990 na kuendelea,ambao sasa umekuwa chachu ya maendeleo kwa vijana wenye vipaji zaidi. Album ya Ni MIMI mwaka 1995 ya mkali Mr II sugu ambaye sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ndiyo album iliyofungua njia ya muziki huu wa kizazi kipya. Na album hiyo kwa mara ya kwanza ilisambazwa na Mzee John Kitime mwaka 1995.

Swala la kukosa album katika muziki wa kizazi kipya limeendelea kushika kasi huku mashabiki nao kuendelea kukosa radha za msanii mmoja kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma. lakini pia sio radha tu pekee hata uwezo wa msanii mwenyewe ni kitu tunachokosa katika muziki sasa.

Zamani wasanii walikuwa wanashindania sana kutoa album utakumbuka kipindi cha Ferooz na Daz Baba,Ngweair na Mchiz Mox,Prof Jay na Mwana Fa pamoja na wengine wengi.

Muziki umebadilika ni hits song tu, maana album haziuzi”hii ni hoja inayotolewa kila siku katika vipindi vya burudani vinavyocheza zaidi muziki wa bongo fleva/hiphop. Lakini je! hoja hii ya muziki umebadilika, ni hoja yenye mashiko?. Maana wasanii wa injili, taarabu na hata bolingo wameendelea kuuza/kufanya biashara ya mauzo ya album mpaka leo hii.

Hoja hii ya album ni hoja pana zaidi ambayo hatutakiwi kuitazama kwa macho ya juu juu huku nikiamini wanaopata nafasi ya kusikika zaidi ndio wanavuruga kwa kuendelea kusambaza hii simu ya album haziuzi.

Siku zinakwenda na miaka ya hivi karibuni tangu 2010-2016 kumekuwepo kwa wasanii wengi chipukizi ambao wameibuka, ukweli ni kwamba wasanii hao walioibuka miaka hiyo ni wasanii ambao wana vipaji vikubwa katika kufanya kazi hiyo ya muziki.

Bahati mbaya waliokutana nayo ni lile jambo la kumezeshwa na walio wachache kuwa Album haiuzi. Lakini je wamewaleleza wasanii hao umuhimu wa kuwa na album?

Umuhimu wa msanii kuwa na album ni msanii kujenga heshima na mizizi katika kazi yake ya muziki (crown and appreciation). Kitendo cha kutoa album hiki ni bora maana hata ukiacha muziki au kutoweka katika uso wa dunia basi wafuasi wako au mashabiki wako hupata kuwa na kazi zako kwa mtindo wa pamoja.

Watu wengi ambao wanafahamu muziki kiundani tokea zamani wamekuwa wakiamini msanii asiyekuwa na album ni msanii chipukizi. Wapo wasanii wanaofanya vizuri katika ramani ya muziki wa kizazi lakini hawana album. Hali hii huonyesha ni wazi bado wanachipukia katika fani chipukizi, pale unatumia kauli za kuaminika kutoka kwa wanaofahamu muziki kiundani. Hii ni kwa maana ya mshabiki kukosa kazi za pamoja za msanii husika yani nyimbo zake kuwa katika album moja. Msanii ataendelea kuwa chipukizi mpaka pale atakapoakamilisha album hata kama utadumu kwa muda mrefu zaidi katika mziki, lakini bila kuwa na album bado utaendelea kuwa chipukizi. Tunao wasanii wengi ambao wana kazi nzuri na wanaendelea kutoa kila siku, lakini hii haitufanyi kuwavika kilemba cha ukoka na kushindwa kuwaambia ukweli kwamba ili wakamiliki katika Sanaa hii lazima watoe na album. Ni sawa na kujiita mtunzi wa vitabu bila kuwahi kutoa kitabu hata kimoja kwa bahati mbaya. Na album unaweza kukusanya nyimbo zako ulizofanya vizuri na kutoa sio lazima ziwe mpya ambazo watu hawajazisikia.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez