Wasanii wa zamani igeni mfano wa Black Rhino.

Wasanii wazamani igeni mfano wa Black Rhino.

Wajuzi wanaamini muziki ni biashara ambayo nyakati zote huuza tena huuza kwa upana mkubwa.

Na wapo wasanii ambao huuza zaidi pale ambapo anapokuwa hayupo katika uso wa dunia.

Yote ni katika uuzo wa biashara ya muziki kwa maana ya muziki hauna nyakati za biashara bali nyakati zote.

Moja ya makosa makubwa wafanyayo wasanii wetu wa zamani kuchukulia urahisi wa bidhaa zao za muziki za zamani na kuona kana kwamba haziwezi tena kuuza.

Hivyo hawana hata fikirio la kuweka nyimbo zao kwa mfumo wa album katika ngazi ya mtandao kwenye tovuti zenye uwezo wa kuuza muziki.

Katika kweli yenye kweli mara zote hunena juu ya mengi ya zamani, na tunaona mashabiki jinsi ambayo wanauhitaji mkubwa nyimbo nyingi za zamani.

Lakini upatikanaji wake si wa rahisi kabisa na zipo nyimbo ambazo hazipo kabisa katika ngazi ya mtandao.

Leo Black Rhino ameamua kuweka Album yake ya ‘Usipime’ iliyotoka mwaka 2007. Album hii yote imewekwa kwenye ngazi ya mtandao na unaipata kwa pamoja.

Jambo hili ni jema mno, na yafaa wasanii wa zamani waige mfano huu wenye maana ya upana wa biashara ya muziki.

Licha ya watu kujua uhalisi wa album iliyopita lakini msanii utaendelea kufaidika na mauzo ya kila leo katika ngazi ya mtandao.

Hakika tunanena tena yakuwa uhitaji wa album zao za zamani kwa mashabiki wa sasa ni mkubwa mno, amkeni wasanii muziki ni biashara katika nyakati zote.

#TuzungumzeMuziki