Wasanii wanawafanya watanzania wajinga.

ce0ca6_fb063fe776f48cec4a780c635ea0923a.png_512

Wasanii wanawafanya watanzania wajinga.

Ni vyema kukumbushana mema katika nyakati hizi ambazo muziki wetu unaonekana kukua kwa kasi nzuri. Lakini kama utakuwa ukikua kwa kasi ya uongo na kufanya mashabiki wajinga haitaleta maana yenye uzuri.

Mashindano ya kupata watazamaji wengi katika mtandao ya Youtube yamekuwa makubwa mno tofauti na miaka kadhaa nyuma.

Imekuwa ni jambo jema katika ushindani na inafanya tupate kazi bora kutoka kwa wasanii wetu wa muziki wa kizazi kipya.

Ila chukizo ni kuona vile baadhi ya wasanii wakiwadangaya watanzania kuwa wameweza kupata watazamaji wengi katika nyakati fupi baada tu ya kuweka video zao kwenye mtandao huo wa “Youtube”

Tumeona ni kawaida katika kurasa zao za mitandao ya kijamii yani Facebook, Twitter, na Instagram kuweka posti zenye kuonyesha mamilioni ya watazamaji huku wakijisifu na maelezo ya ujasiri zaidi. Iko wazi watanzania wapenda muziki huu wamekuwa wakiamini posti hizo, ila wengi wao hawajui ukweli uko wapi katika kupata watazamaji wengi kwa muda mchache tangu kuweka kwa video ya msanii husika kwenye mtandao wa “Youtube”

Katika nafasi ya mitandao yote ya kijamii kuna nafasi ya mtu yoyote kuweza kutangaza kazi yake kwa njia ya kupromote. Yaweza kuwa unaamua kupromote kuanzia upande wa Twitter, Facebook, Instagram na hata Youtube.

Lengo ni kutangaza kazi zao ziweze kuonwa na watu wengi zaidi ulimwenguni kote. Na kitendo hiki cha kupromote huwa si bure, lazima uchangie pesa katika mitandao hiyo ili waweze kuipendekeza video yako itazamwe na watu wengi.

Wasanii wengi sasa wanafanya kitu hicho cha kupromote hivyo hata iweje ni lazima uweze kufikia watazamaji wengi au watumiaji wengi wa mtandao husika. Ila kama hujaweza kupromote kazi yako ni ngumu kufikia watazamaji wengi kwa wakati mfupi. Pia ikumbukwe katika kupromote kazi yako waweza kuwa umeamua ionekana mkoa wowote au nchi yoyote.

Kibiashara ni jambo jema na la kupongezwa kwa kila msanii ambaye anaamua kutangaza kazi kwa njia ya kupromote katika mtandao wowote ule. Ila chukizo ni pale ambapo msanii anajisifu kuwa ameweza kufikisha watazamaji wengi bure kwa kipindi fulani, lakini wakati huo ametangaza kazi yake kwa njia ya matangazo ya mtandao.

Ni ngumu kupata idadi watazamaji hao bure ambao wengi huposti kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii wakijisifu kuwa wamewapata bure. Ni wazi mashabiki wenye upeo mdogo wamekuwa wakitukana wasanii wengine bila kujua njia ambazo anatumia msanii wao. Ni wazi wasanii wanatufanya hatuna akili ila wao hujiona ni wajanja zaidi.

Lakini si kweli kila mtu anaona nguvu ya Digital katika kipindi hiki. Hivyo kufanya watanzania wajinga katika mlengo wa kudanganya ni jambo baya. Tanzania ya leo si ile ya uhuru na mzalendo.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez