“Wasanii wanaangamia/wataangamia kwa kukosa maarifa” Sehemu ya II

Soma sehemu ya I kwanza hapa chini

http://tizneez.com/makala/wasanii-wanaangamiawataangamia-kwa-kukosa-maarifa-sehemu-ya-i/

Endelea sehemu ya II Hapa chini

“Wasanii wanaangamia/wataangamia kwa kukosa maarifa” Sehemu ya II

Huu ni ukweli ambao tunakutana nao kila leo katika jamii ya muziki wa kizazi kipya. Ni jambo la kawaida kabisa kwa msanii kukataa kujibu swali/kuzungumzia jambo katika Radio/Runinga/Blog sehemu hii na jambo hilo akalizungumza katika sehemu nyingine ya Radio/Runinga/Blog.

Ipo mifano  ya wasanii wengi ila Ben Paul na Darasa ni  mifano mipya. “Ukweli utatuweka huru daima” bali uongo utatupa maanguka katika maisha yetu.

Lakini wasanii hawa na wengine wanafanya haya bila kujua kuwa kila Radio/Runinga/Blog inamsomaji/msikilizaji/mtazamaji wake.  Huu ndio uhalisia uliopo katika wasanii walio wengi. Lakini pia wasanii wa aina hiyo hawajui hata takwimu zilizopo sasa juu ya media, ila wengi wamebaki na uzamani ambao wanaujua wao.(Kukarii)

Jambo hili mashabiki hawajui kuwa wasanii wao ni wabaguzi katika kufanya mahojiano na baadhi ya media, mashabiki daima hubaki kulaum watangazaji au dj au media kwa ujumla kuwa hawapigi wimbo wa msanii Fulani au Fulani. Uhalisia si chuki bali ni msanii huyo kukosa nidhamu kwa wafanyakazi au hata media kwa ujumla. Huku msanii akiamini Zaidi katika upande mmoja Zaidi, na upande huo hakika atakuwa mtumwa mara zote.

Wasanii hawa hujiita bora wakati wote. Ilihali  wanasahau msemo usemao “Na tena usijiite bora, kumbuka kwamba hata chuma huchakaa kwa kutu”

Lakini jambo pekee wanalopaswa wasanii wa aina hiyo ni kuwa zama zimebadilika, hivyo yapasa msanii kufanya mahojiano na kile media lakini pia kumuheshimu mtu yoyote ambaye mpo katika njia moja.

“Usiache kumkumbusha mwenzio ukweli, kama tu utaweza kumjenga” ya nini tunyamaze wakati tupo kwaajili ya muziki wa kizazi kipya? Hapana hatuna sababu hiyo.

“Amka msanii kuwa kila media, heshimu kila mtu wa media”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa