“Wasanii wanaangamia/wataangamia kwa kukosa maarifa” Sehemu ya I

“Wasanii wanaangamia/wataangamia kwa kukosa maarifa” Sehemu ya I

“Mshale usiyo na nyoya hauendi mbali” kuna wakati huwa natafakari juu ya misemo ya wahenga na hata kufika hatua ya kukosa namna ya kuchanganua juu ya hekima zao.

Hakika kama utaishi katika hekima zao ni wazi utakuwa tofauti katika maisha haya ya leo, lakini busara itaongezeka kwenye kila jambo ambalo unalifanya.

“Tuzungumze muziki” hii ndiyo ‘slogan’ yetu Team Tizneez, na tupo hapa kwa Bongo fleva/Hiphop yani muziki wa kizazi kipya.

Muziki wa kizazi kipya umeendelea kukua siku baada ya siku, na tunaona mafanikio ya wasanii wengi mno. Team Tizneez kwetu si faraja na furaha kuona mafanikio ya wasanii katika kila upande kuanzia maisha na hata kimuziki.

Ila wimbi la wasanii kuanguka katika muda mfupi pia lipo. Wapo wasanii ambao waliibuka na wakaangamia katika muda mfupi mno.

Sisi hatufurahi juu ya kuangamia kwao, ndiyo maana mara zote huwa tunawakumbusha kupitia maandiko yetu bila kujali jinsi ambavyo watapokea. Maana wengi wanapendwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.

Na jambo hili limepelekea baadhi ya wasanii wamekuwa wagumu kutambua namna ya vyanzo vya maanguko yao.

“Hiari hushinda utumwa” na ukweli huu hatuwezi kuuweka kifuani ilihali mashabiki wanapaswa kujua ukweli ulipo juu ya wasanii walioangamia na watakaoangamia kwa kukosa maarifa, kwa maana yasema “Kama unaujua ukweli halafu unaendelea kuishi kwenye uongo, basi ukweli huo utakuwa hauna maana”

Ni wazi wasanii waliowengi wamekuwa wabaguzi wazuri juu ya watu wa kuwafanyia mahojiano. Wasanii wengi wamekuwa wakiheshimu  baadhi ya watu wachache wa media ila wengine kuwadharau katika mambo mengi.

Huu ni ukweli ambao tunakutana nao kila leo katika jamii ya muziki wa kizazi kipya. Ni jambo la kawaida kabisa kwa msanii kukataa kujibu swali/kuzungumzia….

Itaendelea…..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa