Wasanii wakongwe itumieni Tigo Fiesta kama fursa ya endelezo lenu.

Wasanii wakongwe itumieni Tigo Fiesta kama fursa ya endelezo lenu.

Daima kweli hutuweka huru nyakati zote, hakika furaha yetu ni kubwa juu ya mgawanyo wa nafasi za wasanii wakongwe katika Tigo Fiesta 2018. (Uhalisi)

Jambo hili limeleta chachu nzuri kwa maana ya changanyo la ladha ya burudani kwa maana ya tulipotoka na tulipo kwenye muziki.

Licha ya wasanii wakongwe kuwa na nyimbo nyingi bora za nyakati zote lakini nafasi yao katika matamasha mengi haipo. (Kweli)

Na tazamo la waandaaji wengi wa sasa ni ‘Trend’ zisizo na msingi bila upana na ukubwa wa muziki kwa msanii. (Soni)

Lakini leo hii tunaona Tigo Fiesta 2018 imeweza kuchukua wasanii wengi wakongwe katika ufanyaji tamasha hilo. (Naam)

Ubunifu huu na uamuzi wa Clouds Media Group katika uchukuaji wa wasanii hawa ni mzuri, na tutakuwa ni wanafiki mno kama hatutapongeza uhalisi huu. (Pongezi).

Na rai yetu kwa wasanii wakongwe ni kutumia jukwaa hili kama fursa ya kufanya endelezo la muziki wao.

Maana macho na masikio katika usikivu na tazamo kwa sasa Tanzania ni juu ya Tigo Fiesta si kitu kingine.

Hivyo msanii mkongwe anapaswa kujua yakuwa akifanya tumbuizo lake vyema itamuongezea michongo mingine nje ya Fiesta.

Maana wapo ambao hudhani yakuwa wasanii wakongwe wameishiwa katika ufanyaji tumbuizo.(Hapana)

Jambo la msingi kwa wasanii wakongwe ni kujipanga na kuwa wabunifu katika kila jukwaa ambalo watapanda katika Mikoa tofauti. (Upekee) na isiwe mazoea yaliyopitwa na nyakati.

Pongezi ziwe kwa wasanii wote ambao wameweza kusajiliwa katika Tigo Fiesta 2018, tunaamini mna mengi ya kuonyesha jukwaaani.

Na hakika mnatimiza semi yakuwa “Muziki unaishi nyakati zote, bali hovyo hupita”. Eeh! “Yakale dhahabu”

#TuzungumzeMuziki