WASANII WAJUE GAME YA BONGO HAIOGOPI LAANA WALA LAWAMA.

music

Hakuna kitu kinachoni dissapoint kama kuona kipaji cha msanii ninayemkubali sana kikishindwa kumsaidia kwasababu tu hana adabu wala bidii.

Adabu nazungumzia displine Kuanzia ya kazi yake ,utakuta msanii mkubwa lakini kufanya naye kazi unaanza kujifikiria.MF.ukimwita kwenye interview hawezi kuwa on time au anatoa vijisababu kibao na wengine hata kumpata tu ni kazi.

Msanii tambua game hasa ya bongo haiogopi laana wala lawama.kuna wenye vipaji kibao walishaondoka duniani (R.I.P)wakiwa masikini wa kutupwa na game inaendelea.

Kitu cha msingi msanii alelewe kipaji chako ni 20% tu ya mfanikio yako, zilizobaki zote zinategemea displine na bidii yako ya kazi.

Msanii unakuta PR yako na wasanii wengine ni mbovu una bifu zisizo na maana halafu marafiki zako ni wale ambao hawafanyi vizuri kwenye game.tangu lini kipofu akamwongoza mwezake?

Nakuwa dissapointed sana nnavyomuona msanii wa bongo anashindwa kubadilika ili afanye vizuri kulingana na soko linavyokwenda kwa madai kuwa anasimamia misingi yake.

Msanii inabidi ujitambue kuwa lolote utakalofanya lengo nikutusa na kufanya vizuri kwenye game, sasa kama unajifanya mwanaharakati halafu unashindwa hata kumnunulia mama kanga ya kuvaa hizo ni harakati gani?jiulize vizuri.

Fid Q kwenye ngoma yake Juhudi za wasiojiweza feat bi kidude alisema “aliyechoka kufikiria hujiona anajua sana”. juhudi /bidii

Ukweli ni kuwa tukiamua kuwapanga wasanii wa Tanzania kwa kuzingatia uwezo na vipaji vyao kiuhalisia mfano.waimbaji hapa bongo Usishangazwe kuona no.1 ni msanii ambaye hatujui hata yupo wapi kwa sasa.

Unaweza kukuta wasanii 5 walio juu kimafanikio kwasasa hawapo kwenye list hiyo.kwanini??? Ni kwasabab 80% ya mafanikio yako ni bidii na displine.
Kaka @skytanzania utanisaidia inawezekana ni zaidi ya hiyo %. Nimalizie kusema “Wasanii wajue hakuna media,meneja,mdau wala shabiki yoyote anayejali kupotea kwako hata kama wanakipaji kiasi gani, Utapotea kama walivyopotea wengine, lawama na laana za vipaji vilivyopotea au kupotezwa zishakuwa ugonjwa sugu.

Cc# www.tizneez.com

Instagram@tizneez

Twitter@tizneez

Facebook@tizneez

@batro15

 

 

Source Graysongideon