Wasanii wajifunze kwa Madee, kufanya wimbo na Tekno hakujamsaidia lolote.

Wasanii wajifunze kwa Madee, kufanya wimbo na Tekno hakujamsaidia lolote.

Neno kwenda kimataifa ni wimbo bora uimbwao na kila mmoja ilihali wengi hawajui kwenda kimataifa hakuna uhusiano wowote na msanii kufanya kazi na msanii tokea nchi husika

Kwenda kimataifa ni namna ambavyo utafanya kazi yako kwa ukubwa na tofauti na kile wafanyacho kwa maana ya ladha tofauti na walionayo wao lakini wasikiayo kila leo.

Ipo mifano mingi juu ya wasanii wa zamani ambao waliweza kubahatika kwenda kimataifa tena wakati dunia ni giza bila kuwa na wepesi wa mitandao ya kijamii kama alivyo sasa. Siti Bin Saad ni mfao bora tokea ardhi ya nyumbani.

Ambapo aliweza fanya kazi na Label kama Columbia Records na Master Records. Na alifika huko bila ushirikiano wa wasanii wa nje katika kazi.

Leo katika zama mwanga kwenye mitandao inashangaza kuona msanii/wasanii kuona yakuwa njia pekee ya kufika kimataifa ni kushirikiano na msanii husika wa nchi Fulani.

Ilihali huenda kukawa hakuna mikakati kamili ya namna ambavyo wataweza kuisukuma ile kazi kuweza kufikia mahala pakubwa.

Madee na wimbo wake wa Sikila akiwa na Tekno ambao ulitoka 2017 ni mfano mzuri na hai ambao unaonyesha hali halisi juu ya kwenda kimataifa si kufanya tu kazi na msanii Fulani bali mikakati yenye tija.

Wimbo wa Madee na Tekno haukuweza kufanya vyema kwa mambo kama, kukurupuka yani kufuata upepo lakini mikakati ya namna ya kuutangaza wimbo kuanzia kwenye mitandao lakini kwenye vituo vya radio/runinga vya nchi husika atokayo msanii Tekno.

Ni wazi kufanya wimbo na Tekno hakujamsaidia Madee katika biashara yake ya muziki maana uwekezaji wake katika wimbo huo haukuwa ni wenye mikakati bali msukumo wa muziki yakuwa ni lazima ushirikiane na msanii wa nje.

Lakini gharama ambazo ametumia katika wimbo huo angeamua kuwekeza katika mitandao yake ya kijamii kwa maana ya kupromote kazi zake katika nchi ya Nigeria ni wazi angesogea Zaidi kisanii kuliko kufanya wimbo ambao hakuwa na  mikakati yoyote yenye maana kwa upande wake.

Na wakati wote waswahili husema “Kheri mrama kuliko kuzama”

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa