Wasanii wa zamani wanakwama wapi? (Shangazo)

Wasanii wa zamani wanakwama wapi? (Shangazo)

Uanzo wa siku yetu ni katika usikivu wa wimbo wa T-shirt na Jeans ya University Corner ‘UVC’ ambapo kwa sasa wimbo huu unatimiza miaka 16 tangu kutoka kwake 2003. (Eeh)

Lakini ubora katika usikivu ni ule ule, na haikuwa ngumu kuutafuta katika mtandao wa ‘Youtube’ katika endelezo la kuweka masikio sawa huku kazi za maandiko mengi kuhusu muziki zikiendelea. (Naam)

Lakini jambo baya zaidi wimbo huu haupo katika ukurasa rasmi wa wasanii hawa wa UVC ambapo ni Idrisa a.k.a Dirah na Hasheem. (Kundi)

Na uhalisi ambaye ameweka wimbo huu katika mtandao wa ‘Youtube’ ameendelea kula yaliyomema ilihali hana hata chembe ya umiliki katika wimbo huu. (Soni)

Lakini ikumbukwe si wimbo huu pekee ni nyimbo nyingi kutoka kwa wasanii wengi wa zamani hazipo katika kurasa rasmi za wasanii. Na faida wapatayo watu wengi kupitia wao ni kubwa mno. (Ndiyo)

Kwani katika uhalisia wasanii wa zamani wanakwama wapi? Kwanini hawaweki kazi zao katika mtandao kwa akaunti zao ili waweze kupata chochote kitu kwa maana ni kazi zao zile. (Shangazo)

Unakuta msanii ana album zaidi ya 4 na zote nyimbo zake zipo katika akaunti za ‘Youtube’ kwa watu wengine na yeye yu kimya kabisa akiendelea kuhangaika katika mengi. (Mbaya)

Amka msanii muziki ni biashara ambayo inauza kila leo haina muda kama wasemavyo wengi wasio na ujuzi. Amka msanii ni muda kuweka kazi zako zote katika ukurasa wa wewe na uweze kufaidika kwa upana haswa. (Muda)

Kwanini afaidikie mtu mwingine au watu wengine? Haipaswi kuwa hivyo kabisa, wapo watu wenye uwezo wa kuweka sawa kurasa zenu na muwezi kufadikia na kazi zenu. (Kabisa)]

Sisi tupo kama vivyo kama msanii unahitaji mtu wa kufanya nae kazi ya kuweka nyimbo zako zote katika mtandao wa ‘Youtube’ na ukafaidia usiache kututafuta.

#MuzikiNiSisi

Email tizneez@gmail.com lakini hata dm zetu za kwenye mitandao ya kijamii tutafute.