Wasanii wa zamani mnatafakari nini kuhusu bidhaa zenu za muziki?

Wasanii wa zamani mnatafakari nini kuhusu bidhaa zenu za muziki?

Wajuzi wa muziki hunena yakuwa “Muziki huishi nyakati zote” kwa maana hiyo bidhaa hii ya muziki kila iitwapo siku itaendelea kuhitajika.

Changamoto ipo kwa wasanii wetu wengi wa zamani ambao kwa nafasi yao walifanya makubwa mno kwenye uwanja wa muziki.

Lakini kwa sasa hawafanyi vyema, ila pia wameshindwa kujua yakuwa watu bado wanahitaji bidhaa zao, na hawana pakuzipata katika ngazi ya mtandao.

Ni mara nyingi huandika mengi juu ya nyimbo za zamani, na mashabiki huonyesha namna ya uhitaji wao juu ya nyimbo hizo.

Na wengi huomba tuwatumie kwa email, lakini katika kweli yenye kweli haina maana wala faida kwa msanii husika, nasi hatupendi kuwa moja ya watu ambao husambaza nyimbo za msanii bila faida yoyote kwa msanii.

Hivyo ni vyema wasanii wa zamani mtafakari katika upana wa sasa wa kujua yakuwa muziki ni biashara ya nyakati zote, hivyo mwaweza kuuza vyema sasa.

Ni sawia kabisa kwa wasanii kuweka album zenu zote za zamani katika ngazi ya mtandao katika uuzo wa nyimbo hizo. Maana mashabiki ni wenye uhitaji mkubwa mno.

Na jambo la kuweka nyimbo katika mitandao ya kuuza nyimbo itaendelea kukupa faida wewe msanii kila leo, maana mashabiki wengi hupata kiu kubwa ya nyimbo nyingi za zamani.

Amka msanii! muziki ni biashara ya kila
leo katika nyakati, jambo hili la kuendelea kuuza kazi za zamani hakika itakupa faida kubwa katika usawa wa sasa na muendelezo wako.

#TuzungumzeMuziki