WASANII WA KIZAZI KIPYA WANAJIKWAMISHA WENYEWE

bongoflava

WASANII WA KIZAZI KIPYA WANAJIKWAMISHA WENYEWE

Ni wiki kadhaa zimepita kama sio mwezi/miezi tangu wasanii wa sanaa ya muziki hususani kizazi kipya, walipoamua kutangaza maadhimio yao matatu.Ambayo ni Kuendelea kuchezwa/kupigwa kwa nyimbo zao bure katika vituo vya radio/runinga mpaka watakapotoa tamko, Kuvunjwa kwa bodi ya COSOTA, na la mwisho ni kutokuwa na imani na CMEA.

Sio lengo langu kuyarejesha mawazo ya wengi katika sakata hilo ambalo mpaka sasa bado haijafahamika nini kitafuata baada ya hayo maadhimio maana kumeendelea kuwa kimya na hakuna tena kuzungumziwa kwa nguvu nyingi kama ilivyokuwa siku ilivyotoka tamko la kupinga.(Mashaka)

Team tizneez ilichambua kiundani juu ya maadhimio hayo, na hata baadhi ya wasanii kuona tupo katika mlengo wa kukosoa zaidi kama sio kujenga. Lakini katika uhalisia haikuwa katika kukosoa isipokuwa mlengo wa kujenga na hata kuona mbele yake nini ambacho kitatokea katika muziki wa kizazi kipya. (Kufaidika)

Watu wengi kati ya umri 15-45 wamekuwa wakishabikia muziki huu wa kizazi kipya ambao sasa umekuwa chachu ya maendeleo ya vijana katika angle tofauti tofauti , wapiga picha, watangazaji,dj’s,blog’s, wabunifu wa mavazi, wote wamekuwa ndani ya muziki, maana halisi muziki umekuwa kiasi cha hata kutoa nafasi kwa watu wengi ambao nao wameweza kupata ajira zisizo rasmi, imradi tu mkono uende kinywani. Hapa lazima niisifu Bongo fleva/hiphop hasa kwa waasisi wake wote, ambapo sasa wengi wao hawatajwi wala kuzungumzizwa mchango wao katika muziki huu isipokuwa baadhi ya media zinatumia nguvu kubwa kufuta historia hiyo. (Chuki/Ubinafsi)

Sitaacha kusema/kuandika wakati wote harakati ambazo sasa zinaendelea katika kile kinachoaminiwa kudai haki zao wasanii. Uhalisia harakati hazijaanza mwaka 2015-2016. Isipokuwa harakati za kudai haki zimeanza tangu mwaka 2002-2003 hapa ukweli upo kwa Mzee wetu John Kitime na hata Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi A.k.a Mr II Sugu, ambaye ndiye msanii anaengoza kuwa na album nyingi kuliko msanii yoyote katika bongo fleva/ hiphop mpaka sasa ana album 11

Tizneez ni blog inayoandika kuhusu Bongo Fleva/Hiphop tu, yani muziki wa kizazi kipya, hii naomba ieleweke. Na tupo tofauti na mambo mengi, ila hatuwezi kuwa tofauti katika kuandika ukweli, daima tutasimama kuandika ukweli, maana imeandikwa katika maandiko matakatifu “Ukweli utakufanya uwe huru” wacha tutimize maneno hayo.(Ameni)

Sifa ziwafikie wasanii wote wa kizazi kipya mnaoendela kupigania haki zenu, mafanikio mlinayo mnapaswa kuwa zaidi ya hapo mlipo.”Amkeni”

Kuna mengi inabidi tuendelee kukumbusha katika kila iitwapo leo, harakati katika kudai haki zimekuwa tofauti na nyakati za miaka ya nyuma. Miaka hii wasanii wameweza kukutana kiurahisi zaidi. Licha ya kukutana ila uwezo wa uchangiaji wa mawazo unaweza fanywa hata kwa njia ya simu, mfano katika magroup ya WatApps na hilo nawapongeza. “Hongereni”

Lakini je kwenye group la WatApps “wasanii tz” mpo wasanii wenyewe kweli? Hapa ndipo ninaona wazi mnajikwamisha katika mambo yenu mazuri mnayopanga ili muweze kuokoa yaliyomengi katika muziki wenu. Na kama hampo wenyewe hamuoni kama mnatoa nafasi ya watu wasiohusika kujua mawazo yenu mazuri mnayopanga?

Pengine watu wengi hatuna uwezo wa kuona ukweli kama unavyojionesha na badala yake tunaona ukweli kama ni ubaya katika maisha yetu. Tusifichane katika kujenga ukweli kusema ukweli, kwenye ukweli tuwe wa kweli “Ukweli”

Kuna wale mnaowaita wadau wa muziki, hivi katika group lenu au vikao vyenu wasanii hao wadau wanakuja kuchangia/kufanya nini? Kweli hao wadau wana lengo moja na wasanii? Hawapo kujua kile mnachopanga? Na kwenye vikao vyenu wanataka nini? Kweli hamjui kama mdau/wadau ana matatizo na baadhi ya wasanii? Sasa anahusika vipi katika maswala ya kujenga sanaa yenu? (Tatizo)

Hili sio jambo la kuficha kati ya mdau na msanii, katika uhalisia na ukweli wapo wadau ambao wana matatizo binafsi na wasanii wengi tu. Wapo wasanii waliwahi hata kuthubutu kusema juu ya wadau kadhaa kuwa ni vinara wa kupora haki za wasanii, Je leo hii wadau kuwepo katika umoja wa vikao na hata hayo magroup kuna uwezekano wa wasanii wengine kuchangia katika mawazo? (Fikiri)

Kichekesho ni pale mdau anapokuwa na maamuzi/mamlaka makubwa kwenye group/vikao vya wasanii hata ya kutaka msanii Fulani atolewe kwenye group ambalo ni la wasanii tu. Hii hainipi maana nzuri, haikuwa sawa kwa mdau mmoja kumtoa msanii nadhani ingeleta maana kufanya hivyo katika group lake la wasanii wake ambapo huko watapanga mambo yao binafsi, lakini si sawa katika group lililojaa wasanii tofauti. (Uoga)

Siamini katika urafiki wa paka na panya hata mara moja. Hapa napata kutafakari zaidi ya mara tatu, kwani wadau na wasanii wanapigania kitu kimoja? Maana wasanii wanapigania kupata haki zao kama vile malipo ya mirabaha na mengine mengi. Mdau/wadau je wanapigania jambo gani? Sasa mbona wapo katika group/vikao na wasanii?

Hofu imetawala kwa wasanii walio wengi ambao ni wazi wanaamini hawataweza bila mdau Fulani, hakika hiki ni kitanzi kinachonyonga sanaa ya muziki wa kizazi kipya kama sio wasanii husika “Hofu”

Ivueni hofu mlinayo kati yenu, kaeni muamini mnauwezo , nyinyi ndio mnamuweka mdau na sio mdau kuwaweka nyinyi. Hakuna mdau kama hakuna msanii, ila kuna msanii hata kama hakuna mdau. Kuna wasanii wengi hawapo karibu na mdau/wadau na tunaendelea kuwasikia wakifanya vyema. Rama Dee ni mfano tosha katika hili.”Ivue hofu”

Ni vyema mambo yanahusu wasanii yafanye na wasanii wenyewe husika, naamini kuna mafanikio mengi kama mtasimama wenyewe na kujitetea wenyewe. Lakini kama mdau/wadau watakuwepo ni wazi haitakuwa rahisi kuwa na umoja na hata kupata mafanikio katika kile mnachokipigania.”Simama”

Katika andiko la kikao cha wasanii cha kisanii niliwahi sema “Unajifungia ndani na adui halafu unaeleza mbinu zako vile ambavyo unajilinda” ni wachache ambao walielewa maana ya sentesi hii.

Uache ukweli ujitenge na uongo daima. Ni vyema kusimama katika ukweli maana utaheshimika isipokuwa uongo utadharaulika baada ya muda mfupi.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez