“Wasanii wa hiphop ni vipofu wa mitandao ya kijamii”

“Wasanii wa hiphop ni vipofu wa mitandao ya kijamii”

Iko wazi nguvu ya hiphop  ni kubwa juu ya muziki wote katika majukwaa yote. Hili hulidhihirika pale tu kunapokuwa na tamasha lolote lile nguvu ya muziki wa hiphop na wasanii wake huwa kubwa mno, na hii ni hata kama msanii husika ataimba wimbo wa zamani basi shangwe huwa ni kubwa kupita kiasi.

Muziki umekua ni kauli pendwa kwa wasanii wengi wa hiphop ilihali hawaendi sawa na kauli hiyo.

Ni kweli muziki umebilika katika mambo mengi kulinganisha na zamani. Leo msanii yoyote yule anaweza kuachia wimbo kwenye mtandao tu na wimbo huo ukapata kuwa mkubwa kwa jamii yote.

Ukubwa wa wimbo huwa kulingana na namna ya nguvu ya msanii husika vile ambavyo ataamua iwe katika mitandao hiyo ya kijamii.

Wasanii wengi wa hiphop ni vipofu katika kutumia mitandao ya kijamii kutangaza kazi zao. Kutumia mtandao wa kijamii sio kuposti picha tu au kuandika chochote wakati wote juu ya wimbo wako, bali katika kutumia vyema kutangaza kazi yako mpya au hata kazi yenye maana Zaidi na yenye uhitaji wa kuonekana kwa ukubwa wakati huo.

Wasanii wa hiphop mara zote wamekuwa wepesi wa “Naomba unisaidie kushare” ilihali wanashindwa kujua yakuwa anaweza kutumia ukurasa wake wowote katika mtando wa kijamii katika “Kupromote” ili kazi hiyo ionekana na watu wengi Zaidi tena katika fumo wa kuchagua eneo atakalo.

Hivi wimbo kama wimbo wa  Zimbambwe wa Roma au wimbo wa Kata Leta wa Joh Makin akiwa na Davido  wangeweza kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii katika “Kupromote” hakika nyimbo hizi zingeweka rekodi za pekee katika muziki wa hiphop.

picha chini ya Ali Kiba na Diamond Platnumz wakiwa wamepromote kazi zao ili kuweza kufikia/kutangaza kazi zao zaidi.

Lakini licha ya rekodi zingekuwa daraja zuri la kuwavusha katika kuwapeleka wasanii hawa mbali Zaidi katika uwanja wa Africa nzima sasa.

Hivi tutafakari ukubwa alionao Casper Nyovest kutoka Afrika ya Kusini ambaye ni msanii anaeweza kujaza uwanja wa mpira kwa shoo yake , lakini bado akiwa na wimbo mpya hutumia mitandao ya kijamii kupromote kazi yake hiyo.

Sasa kipi kinafanya wasanii wetu kuwa vipofu katika hili? Ni wazi tukisema muziki umekua ni vyema kwenda na kasi hii nzuri na ya maana katika nyakati za sasa.

Na kwa mapenzi yetu ya hiphop tunaweka wazi kwa msanii yoyote wa hiphop ambaye atapenda kazi ya iwe “Sponsored”kwenye mitandao yote ya kijamii basi Tizneez tunajua namna ya kufanya jambo hilo. Hatuhitaji malipo kwa hili tunafanya kwa kukuza na kuendeleza vyema Bongo Hiphop.

#ZimaKikiWashaMuziki.

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa